Gor Mahia yafuzu kwenye awamu ya robo fainali za CECAFA

Mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya Gor Mahia wamefuzu kwenye hatua ya robo fainali za Kagame Cup. Ko'galo walifuzu kwenye hatua hio huku wakiwa na mechi moja mkononi kwenye awamu ya makundi.

Gor Mahia ilicharaza Ports FC magoli mawili bila jibu kwenye mechi yao ya pili ya kundi D. Mshambulizi mpya wa Gor Mahia alicheka na wavu jambo lililomsisimua kocha mkuu Hassan Oktay aliyesema kuwa anafurahishwa na wachezaji wake wapya.

Kwa sasa,Gor Mahia mahia imejiunga na Rayon sports pamoja na APR  ya Rwanda kwenye hatua ya robo Fainali za msimu huu.

Mabingwa watetezi Azam walipoteza mechi yao ya pili jana walipo nyukwa goli moja kwa nunge na Kampala FC ya Uganda. Azam itachuana na Bandari walio katika nafasi ya tatu na alama mbili kwenye mechi yao ya mwisho. Iwapo watapoteza basi bandari itatinga kwenye hatua ya robo fainali.