Tumechoka! Mashabiki wa Arsenali waungana mkono kukashifu uongozi

Baada ya msukosuko wa matokeo duni msimu uliopita, mashabiki wa Arsenal wamejitolea na kuungana mkono kukashifu viongozi wa klabu hio.

Mashabiki hao walimwandikia mmiliki wa timu hio barua kuweleza hasira zao huku wakielekeza lalama zao kwake Kroenke. Kroenke ndiye mimiliki mkuu wa Arsenali.

Kwenye barua hio, mashabiki wa Arsenal wanalikashifu tendo la Mwenyekiti kushindwa kuleta bodi itakayofanya usimamizi wakati yeye hayupo.

Pia, mashabiki hao wamelalama kuhusu tiketi za hali ya juu wanazotozwa pamoja na umiliki mbovu wa tiketi zenyewe haswa wakati wa mechi kubwa.

Wakati Kroenke alinunua klabu ya Arsenali, timu hio ilikuwa imetoka kumenyana katika fainali ya klabu bingwa barani ulaya. Hata hivyo, misimu  mitatu iliyopita Arsenali imejipata katika nje ya michuano ya Europa League.

Kufuatia msururu wa matokeo duni msimu uliopita, Arsenali sasa itacheza mechi za Europa league msimu ujao.

Mashabiki wa Arsenal pia wamesisitiza kupewa habari iwapo timu yao itajiunga na mashidano mapya ya UEFA yanayotarajiwa kufanyiwa uchaguzi mwezi disemba mwaka huu.

Pamoja na hayo, Mashabiki  hao wameieleza klabu kufanya sajili zitakazo leta raha na msissimko msimu ujao ugani Emirates.

"Arsenal have invested money in recent years, but their approach to both buying players and paying wages looks uncoordinated and appears to lack strategy. There has also been a lot of turnover in the senior football personnel. A strong board would be proactively managing this."

Barua ya mashabiki inawaomba viongozi wa klabu hio kutoa habari zaidi mnamo tarehe 25 wakati wa mkutano baina ya wamiliki na mashabiki kadhaa waliochaguliwa.