Orodha ya makocha waliofutwa kazi baada ya AFCON

seedorf
seedorf

Herve Renard anajiuzulu kama kocha mkuu wa Morocco baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika kashindani ya kombe la mataifa ya Afrika.

Morocco ni mojawapo wa timu zilizopigiwa upatu kabla ya kuanza kwa mahsindano hayo Misri 2019 lakini ilishindwa kupitia mikwaju ya penalti na Benin katika timu 16 za mwisho.

Renard, raia wa Ufaransa amewahi kushinda mataji mawili ya Afcon na Zambia (2012) na Ivory Coast mnamo 2015, alikiongoza kikosi cha Morocco tangu Februari 2016.

"Umwadia wasaa wa mimi kuufunga ukurasa huu mrefu na mzuri katika maisha yangu," amesema Renard mwenye miaka 50.

Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii, Renard amesema "Ni uamuzi usioweza kuepukika ulichukuliwa hata kabl aya kuanza mashindano ya Afcon 2019.

"Nilichukua uamuzi huu- bila shaka - baada ya kutafakari kwa makini. kwahivyo siwezi kuugeuza."

Renard aliitoa Morocco kutoka nafasi ya 81 katika orodha ya Fifa duniani hadi katika nafasi ya 47.

Hatahivyo Renard siyo kocha wa kwanza kuondoka au kuondolewa kutokana na matokeo duni katika mashindano hayo yaliokamilika mwaka huu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mapemamwezi Julai limetangaza kusitisha mkataba na kocha Emmanuel Amunike.

Taarifa fupi iliyotolewa na TFF inadai kuwa Amunike amekubaliana na TFF kusitisha mkataba huo.

"Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019," ilisema taarifa ya TFF.

Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018.

Atabakia kwenye historia ya mpira Tanzania kwa kuingoza nchi hiyo kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya miaka 39.

Kabla ya hapo alinyanyua Kombe la Dunia 2015 akiwa kocha wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 Nigeria.

Kocha huyo ni winga wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Barcelona.

Hata hivyo, Amunike amekuwa akilaumiwa na baadhi ya mashabiki kwa namna anavyoteua wachezaji na kupanga kikosi.

Tanzania ilitolewa katika mashindano ya Afcon baada ya kupoteza michezo yote ya makundi.