Harambee Stars yabanduliwa kwenye michuano ya Chan na Tanzania

7b41bfe89e6713da8249b966779ea5b3
7b41bfe89e6713da8249b966779ea5b3
Timu ya Taifa ya Harambee stars ilibanduliwa kwenye michuano ya Chan na Tanzania baada ya kucharazwa magoli manne kwa moja kupitia njia ya penalti.

Mechi hio ilikamilika sare tasa baada ya dakika tisini kwenye mkondo wa pili baada ya sare tasa nyingine wiki iliyopita mjini Dar-es- salaam.

Mlinda lango wa Tanzania, Juma Kasaja aliibukia kuwa gwiji kwenye mchezo huo baada ya kupangua matuta mawili ya penalti kutoka kwa Mike Kibwage pamoja na Joash Onyango.
Clifton Miheso aliifungia Kenya penalti ya kipekee huku Erasto Nyoni, Paulo G0dfrey, Gadiel Michael pamoja na Hamisi wakicheka na wavu upande wa watanzania.

Mwezi Juni Stars ilibwaga Tanzania kwenye Mechi za AFCON magoli matatu kwa mawili huku raudi hii stars ikikosa ukakamavu na utulivu kwenye mechi hio.

"Tulipewa kila kitu na shirikisho ila tumeshindwa kuonyesha makali yetu kwenye mechi ya leo. Naamini kuwa kikosi hiki kina uwezo mkubwa wa kuliwakilisha taifa la Kenya'' Migne alisema.