Kocha wa Harambee Stars amethubutu FKF kumfuta kazi

sebastien.migne
sebastien.migne
Kocha wa Harambee Stars Sebastien Migne amelithubutu shirikisho la soka nchini FKF kumfuta kazi akihoji kwamba haamnini kuwa rais Nick Mwenda anaweza kumudu matokeo ya uamuzi kama huo.

Migne ameongea haya baada ya Kenya kubanduliwa kutoka kwa michuano ya kufuzu kwa CHAN mwaka 2020 baada ya kupoteza 4-1 kwa Tanzania. FKF italazimika kumlipa Migne shilingi milioni 50 iwapo itamfuta kazi. Baadhi ya wakenya wanamtaka kufutwa kazi baada ya matokeo hayo duni.

Mshambulizi Dennis Oliech ametajwa katika kikosi cha Gor Mahia kitakachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa ya Caf kwa msimu wa mwaka 2019/20.

Oliech, ambaye alikosa sehemu kubwa ya msimu uliopita kutokana na jeraha la mkono amejumuishwa katika kikosi cha washambulizi wanaojumuisha wachezaji wageni Dickson Ambundo, Gislain Gnamien, na Francis Afriyie. Kinda Eliud Lokuwom na Erick Ombija, pamoja na Kennedy Otieno ambaye alisajiliwa majuzi kutoka Western Stima hawakujumuishwa.

Kwingineko, Manchester United wameafikiana kwa mkataba wa usajili wa mwaka mmoja wenye thamani ya pauni milioni 6.2 na mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic mwenye umri wa miaka 33.

Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia huenda pia akafikia gharama ya karibu pauni milioni 15 au atakuwa sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na mshambuliaji wa United na Ubelgiji, Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 26.

Derby County wanaripotiwa kuwa katika majadiliano ya kumsajili aliyekua kiungo wa Manchester United Wayne Rooney kutoka DC United.

Rooney anatarajiwa kusafiri hadi Midlands kujadili mkataba huo. Bado ana miaka miwili iliyosalia kwenye mkataba wake na DC United lakini inakisiwa kwamba kuna mipango ya kuufuta mkataba huo na kumruhusu Rooney kuregea Uingereza.