'Sonko alisema ukuje na ile safi,' wakenya wambia Uhuru

Wakenya hawakomi kusema sema na raundi hii wameamua kumkumbusha rais Uhuru Kenyatta mambo asiyofaa kusahau akirejea humu nchini akitoka nchini Jamaica aliko kwa ziara yake ya siku tatu.

Kwenye mtandao wa kijamii, wakenya wamempa rais wao mahitaji fulani atakapokuwa nchini jamaica.

Baadhi ya maoni yakionekana kulenga utumizi wa bhangi kama dawa humu nchini. Jambo hilo limezuka wakati ambapo taifa limo kwenye mjadala wa iwapo ni vyema kufanya utumiangi wa bhangi uwe halali.

 Uhuru alikuwa mgeni wa heshima kwenye hafla ya 67 ya ukulima ya taifa la Jamaica iliyofanyika siku ya jumanne mjini Kingston Jamaica.

Sido Muhando: Sonko alisema unarudi na ile kitu safi! Tunakuaminia, #LegaliseIt"

LilKoima:we stand a HIGH chance of legalizing something with HIGH medicinal value!"

Cornel Reborn Muli:Uhuru ambia serikali ya Jamaica imwachilie Vybz Kartel aliyekamatwa kwa madai ya kuuwa watu.

Kipkeleny Tulwo: Tunangojea gunia la kwanza la bangi lifike humu nchini ili tuweze kulingojea airport kama makomada wa polisi tukiwa na mabunduki.

Lazo:Tafadhali waeleze tunataka ndege ya moja kwa moja kutoka Jamaica hadi Kenya.

Pamoja na hayo,wakenya walizidi kuyatumia maneno ya kimuziki ya nyimbo aina ya reggea kama vile Wallan Shutter na big ting wagwana.