Bayern Munich wapanga kumsajili Philippe Coutinho kwa mkopo

coutinho (1)
coutinho (1)

Bayern Munich wanataka kumsajili Philippe Coutinho kwa mkopo, iwapo hawatahusika katika mpango wa kubadilishana na Paris Saint-Germain ambao utahusisha Neymar kuregea Barcelona.

Klabu hiyo ya Bundesliga wanatazama kwa karibu majadiliano kuhusu Neymar kati ya Barcelona na PSG na iwapo Coutinho hatahusishwa kwenye mkataba huo watawasilisha ofa juu yake.

Barcelona wamemwekea raia huyo wa Brazil thamani ya pauni milioni 80 na wangependa kumuona Coutinho akiondoka Nou Camp kwa uhamisho wa kudumu.

Aliyekua mlinzi wa zamani wa Gor Mahia Karim Nizigi-yimana anasema yuko tayari kufanya vyema na klabu yake mpya ya Wazito FC. Mzaliwa huyo wa Burundi mwenye umri wa miaka 27 alihama KO’gallo mwaka uliopita na kujiunga na Vipers ya Uganda baada ya kusaidia kushinda mataji manne ya ligi.

Karim pamoja na mwenzake Abouba Sibomana ambaye pia amejiunga na Wazito walijiunga na Gor mwaka wa 2015 kabla ya kuondoka miaka miwili  baadae kuelekea Rwanda.

Timu za Kenya zinazojitayarisha kuiwakilisha nchi katika mashindano ya All Africa Games huko Moroco jana zilifurushwa kutoka kwa hoteli walimokua wakikaa kwa zaidi ya lisa limoja kutokana na kutolipwa kwa malazi yao.

Malkia Strikers na wanariadha walikua miongoni mwa waliofurushwa huku mizigo yao ikizuiliwa. Hata hivyo waliruhusiwa kuregea kwenye vyumba vyao baada ya serikali kuingilia kati. Malkia wanatarajiwa kuondoka kuelekea Morocco kwa makundi mawili huku la kwanza likiondoka kesho tarehe 15 na la pili tarehe 16.

Shirikisho la mpira wa vikapu nchini limeahidi kumaliza kulipa marupurupu ya timu ya kitaifa ya kinadada watakaporegea nyumbani kutoka kwa michuano ya ubingwa Afrika huko Senegal. Hii ni baada ya timu hio kuiomba serikali kuingilia kati. Haya yanajiri wakati mechi yao dhidi ya Angola inakumbwa na shaka huku wachezaji wakitishia kuisusia. Timu hio iliondoka nchini na wachezaji wachache kutokana na uhaba wa fedha.

Malamishi kuhusu kucheleweshwa au kutolipwa marupurupu ya wanamichezo wanaowakilishi nchi katika mashindano ya kimataifa ni jambo la zamani, kulingana na katibu katika wizara ya michezo Peter Kaberia.

Akiongea wakati wa kuiaga timu ya Judo kambini Kaberia anasema wameanza mfumo mpya unaoambatana na mwongozo wa tume ya mishahara na malipo SRC.

Katibu huyo pia amepuuzilia mbali malalamishi kutoka kwa baadhi ya shirikisho za spoti kuhusu idadi ya nafasi za kusafiri zilizowekewa wanamichezo wao. Shirikisho la Taekwondo lilikuwa linataka kuongezwa kwa nafasi za wanamichezo watakaosafiri hadi Morocco.