Jesse Were arudishwa kwenye kikosi cha Harambee stars

Kocha mpya wa Harambee stars, Francis Kimanzi amemrudisha mshambulizi Jesse were kwenye kikosi cha Harambee stars kitakacho menyana na Uganda kwenye mechi ya kirafiki mnamo tarehe 8 mwezi septembar mwaka huu. Were alitia wavuni magoli ishirini na mawili chini ya uongozi wake Francis Kimanzi wakati akivalia jezi ya Tusker FC mwaka 2015.

Aliyekuwa kocha wa Harambee stars, Sebastiane Migne alikuwa hapendezwi na uchezaji wake Were ila kocha Kimanzi anaamini kuwa were ni mmoja kati ya washambulizi hatari mbele ya lango. Hata hivyo, Mlinzi David Owino, Anthony Okumu pamoja na Musa Mohammed wameachwa kwenye kikosi hicho. Mike Kibwage, Kenneth Muguna, Samuel Olwade, Boniface Muchiri pamoja na Moses Mudavadi wameitwa kwenye kikosi kwa mara ya kwanza.

 Walindalango

Patrick Matasi (St. George SC, Ethiopia), John Oyemba (Kariobangi Sharks, Kenya), Faruk Shikalo (Young Africans SC, Tanzania)

Walinzi.

Joseph Okumu ( Real Monarchs FC, USA), Mike Kibwage (KCB FC, Kenya), Joash Onyango (Gor Mahia FC, Kenya), Benard Ochieng (Wazito FC, Kenya), Abud Omar (Sepsi OSK Sfantu Gheorghe, Romania), Erick Ouma (Vasalunds IF, Sweden) Nicholas Meja (Bandari, Kenya), Samuel Olwande (Kariobangi Sharks, Kenya)

 Viungo
Victor Wanyama (Tottenham Hotspurs FC, England), Francis Kahata (Simba SC, Tanzania), Boniface Muchiri (Tusker FC, Kenya), Kenneth Muguna (Gor Mahia FC, Kenya), Duke Abuya (Kariobangi Sharks FC, Kenya), Ismael Gonzales (UD Las Palmas FC, Spain), Clifton Miheso (Gor Mahia FC, Kenya), Johanna Omolo (Cercle Brugge, Belgium), Ayub Timbe (Beijing Renhe FC, China), Cliff Nyakeya (FC Masr, Egypt), Erick Johanna (IF Brommapojkarna, Sweden), Moses Mudavadi (Kakamega Homeboyz FC), Whyvone Isuza (AFC Leopards SC)
 Washambulizi

Michael Olunga (Kashiwa Reysol FC, Japan), Jesse Were (Zesco United, Zambia), John Avire (Sofapaka FC, Kenya)