Neymar amekubali kusalia PSG baada ya mazungumzo ya kuregea Barcelona kutibuka

Neymar amekubali kusalia PSG baada ya mazungumzo ya kuregea Barcelona kutibuka. Anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha Brazil hii leo huko Miami kabla ya mchuano wao wa kirafiki dhidi ya Colombia Septemba tarehe 6th.

Neymar ananuia kuheshimu salio la mkataba wake PSG. Kudinda kwa timu hio kushukisha thamani yake licha ya Neymar kutaka kulipa zaidi ya pauni milioni 17 ili kufanikisha mkataba, kulisababisha majadiliano hayo kutibuka.

Liverpool ilisalia kileleni baada ya kuwanyuka Burnley mabao 3-0 jana. Sadio Mane na Robertom Firmino waliongezea bao la  Chris Wod la ufunguzi na kuifanya the reds kuwa timu pekee iliyo na rekodi ya asilimia 100.

Kwingineko mabingwa Manchester City waliwacharaza Brighton 4-0 na kusalia katika nafasi ya pili alama 10 nyuma ya Liverpool. Manchester United nayo ilitoka sare ya 1-1 na Southampton huku Chelsea pia wakitoka sare ya 2-2  na Sheffield United.

Mabingwa wa KPL Gor Mahia walianza utetezi wa taji lao kwa kuwanyorosha mahasimu Tusker  5-2, katika uwanja wa Kisumu jana.

Nahodha Kenneth Muguna alifunga magoli mawili huku Nicholas Kipkirui, Charles Momanyi na Boniface Omondi wakiongeza goli moja kila mmoja.

Boniface alifungia wanamvinyo mabao mawili ya kufuta machozi.  Katika uwanja huo huo Enosh Ochieng alifungia  Ulinzi Stars mabao mawili na kuwalaza wenyeji  Kisumu All Stars 2-0.

Ugani Awendo, Enoch Agwanda, Stephen Waruru na Dennis Odhiambo walicheka na nyavu na kuwanyuka wenyeji  Sony Sugar 3-0 na kusalia nambari mbili kwenye jedwali nyuma ya Ko’gallo.  Wazito nao walitoka sare ya Nzoia United huku Mathare United na Bandari wakiumiza nyasi kwa sare tasa.

AFC Leopards itapambana na Kakamega Homeboyz katika mechi yao ya ufunguzi ya ligi ya KPL, huku pande zote mbili zikitafuta ushindi. Kocha wa Ingwe Andre Mbungo anatumai washambulizi wake watafunga magoli baada ya kulegea katika mechi nne zilizopita. Homeboyz nao watakua wanatarajia mshambulizi mkongwe Allan Wanga atafunga magoli. Katika mechi nyingine Zoo Kericho itacheza na Chemilil Sugar katika uwanja wa Kericho green stadium. Mechi zote zitaanza tisa kamili.

Arsenal na Tottenham watapambana katika North London derby ugani Emirates kwanza 6.30 jioni, huku pande zote zikitafuta alama tatu baada ya kupoteza wikendi iliyopita.

Arsenal watamkaribisha Mesut Ozil kwa mara ya kwanza msimu huu, huku kiungo wa Tottenham Dele Alli pia akirejea kutoka jeraha. Hata hivyo Kyle Walker atakosa  mechi hio kutokana na jeraha. Wolves  pia watakua wanatafuta ushindi wao wa kwanza msimu dhidi ya Everton mweno wa 4pm, baada ya kuandikisha sare tatu msimu huu.