Kumewaka moto: Wachezaji wa Spurs wakasirishwa na matamshi ya kocha

Wachezaji wa Spurs wamekasirishwa na mkufunzi Mauricio Pochettino baada ya kusema kwamba walikuwa na ajenda tofauti wakati waliposhindwa na Colchester katika kombe la Carabao siku ya Jumanne.

Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, huku Spurs ikijiandaa kutokosa huduma za kiungo huyo wa Denmark katika uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu.

Paul Pogba ameiomba Man United kumpatia kandarasi mpya yenye thamani ya pauni laki sita kwa wiki. Kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 26, anajua kwamba ananyatiwa na Juventus pamoja na Real Madrid.

Mkufunzi wa Jose Mourinho anataka kurudi Real Madrid, baada ya kukataa ofa kutoka Monaco, Lille, Wolfsburg na AC Milan tangu alipofutwa kazi na klabu ya Manchester United mwaka uliopita.

Mkataba wa sare mpya ya Liverpool inayodhaminiwa na kampuni ya sare za michezo una thamani ya pauni milioni 15 kwa mwaka ikilinganishwa na mktaba wao sasa na kampuni ya New Balance, ambayo inatoa pauni milioni 45 kwa mwaka.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kwamba hana wasiwasi kuhusu hali ya kiungo wa kati wa timu hiyo James Milner, 33, kuwa katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake .

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 31, ametoa ishara ya kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya River Plate kandarasi yake itakapokamilika 2021.