Soma jinsi serikali ya Misri ilivyowaokoa Harambee Stars mjini Cairo

harambee stars
harambee stars
Serikali ya Misri iliwaokoa Harambee Stars waliokua nusura wafurushwe kutoka kwa hoteli yao jijini Cairo kutokana na kutolipwa kwa ada.

Stars wako jijini humo kwa mechi yao ya kufuzu kwa AFCON ya kundi G dhidi ya the Pharaohs leo usiku. Rais wa FKF Nick Mwendwa ameilaumu serikali kwa hali hio ambayo anasema inatishia kusambaratisha mechi yao dhidi ya Misri.

Serikali hata hivyo kupitia kwa katibu wa michezo Kirimi Kaberia ilirushia lawama FKF huku Kaberia akisema hawakuipa serikali taarifa muhimu na kuwa walitaka kupewa pesa taslim.

Harambee Starlets wamewasili salama nchini Tanzania kabla ya kipute cha ubingwa wa kinadada cha CECAFA mwaka 2019 kinachopangiwa kuanza jumamosi.

Hii ni siku moja tu baada ya kinadada hao kuwasili nchini kutoka Zambia ambapo walibanduliwa nje ya michuano ya kufuzu kwa olimpiki ya bara mwaka 2020 na She Polopolo.

Starlets wanatumai kushinda taji hilo ambalo limekua likiwaponyoka katika miaka ya hivi majuzi, watakapoanza kampeni yao dhidi ya Ethiopia jumapili tarehe 17.

Meneja wa Uingereza Gareth Southgate anasema hatasita kumchagua kiungo Raheem Sterling kwa mechi ya jumapili ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 huko Kosovo.

Sterling alichujwa kutoka kwa mechi ya leo baada ya kulumbana na mwenzake Joe Gomez. Uingereza inahitaji alama moja tu dhidi ya Montenegro ili kufuzu. Sterling anayechezea Manchester City Sterling atacheza mechi ya jumapili huko Kosovo.

Wing'a wa Chelsea Callum Hudson-Odoi anasema aliongea na meneja Frank Lampard kumshawishi asalie Stamford Bridge. Kinda huyo wa miaka 19 aliwasilisha ombi la kutaka kuhama mwezi Januari baada ya Chelsea kukataa ofa ya pauni milioni 35 kutoka kwa Bayern Munich.

Hata hivyo Odoi amemfurahisha Lampard aliyechukua uskani msimu wa joto. Odoi atakosa mechi za msimu huu baada ya kupata jeraha la mguu alipokua akicheza katika mechi yao dhidi ya Burnley mwezi Aprili.

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaregea katika ulingo wa soka baada ya kukubali kuwa mkuu wa ukuzaji soka duniani wa FIFA. Hatua hii inamaliza uvumi uliomhusisha mfaransa huyo na kurudi kama meneja wa Bayern Munich.

Wenger aliondoka Gunners Mei mwaka 2018, baada ya miaka 22 mamlakani. Wadhfa wake mpya utasaidia kukuza soka ya kinadada na wanaume na vilevile masuala ya kiufundi.