Huduma ya polisi yampongeza Omanyala kwa kutwaa dhahabu Mauritius

Muhtasari

•Omanyala aliibuka mshindi kwa sekunde 0.003 mbele ya mpizani wake wakaribu Akani Simbine. 

•Amerodheshwa kama mkenya wa pili kushinda taji ya medali katika mbio za kilomita mia moja baada ya shujaa Joseph Gikonyo.

Ferdinand Omanyala
Ferdinand Omanyala
Image: HISANI

Kitengo cha Huduma ya polisi kimepongeza mwanariadha Ferdinand Omanyala kwa kushinda medali katika mashindano ya Africa Senior Athletic Championship yaliyofanyika Reduit, Mauritius.

Omanyala alifanikiwa kuondoka na medali ya dhahabu baada ya kuwabwaga wapinzani wake wote katika mbio za mita 100.

Omanyala ambaye ndiye anayeshikilia rekodi ya Afrika katika mbio za mita mia moja kwa upande ya wanaume bara la Afrika, aliibuka mshindi kwa sekunde 0.003 mbele ya mpizani wake wa karibu Akani Simbine. Alimaliza mbio hiyo kwa sekunde  9.927.

Mwanariadha alivuja rekodi ya mwanariadha kutoka Nigeria  Seun Ogunkoya ya  9.94 sekunde ambayo aliweka mwaka wa 1998.

Amerodheshwa kama mkenya wa pili kushinda taji ya medali katika mbio za kilomita mia moja baada ya shujaa Joseph Gikonyo.

Omanyala ameweka wazi kuwa lengo lake kuu ni kuvunja rekodi ya dunia ambayo kwa sasa inashikiliwa na Usian Bolt wa Jamaica.

Alivunja rekodi ya Afrika mwezi Septemba mwaka jana baada ya kumaliza mbio hizo kwa sekunde 9.77 wakati wa  Kip Keino Classic Tour .

"Rekodi ya dunia sio ya kipekee na hakuna lisilowezekana katika ulimwengu huu. Naamini itavunjwa na wa kuivunja ni mimi maana hakuna aliyeamini kuwa Mkenya anaweza kukimbia haraka," Omanyala alisema katika mahojiano na BBC.

Mwanariadha huyo alisema kuwa hakuwahi kufikiria angefikia hatua ambayo ameweza kufikia sasa.