ASANTE

Chepngetich awashukuru mashabiki kwa kumtia moyo

Chepngetich aliahidi kuvunja rekodi katika mbio zake zijazo.

Muhtasari

Chepngetich alifanikiwa kutetea taji lake katika kinyang'anyiro hicho baada ya kuvunja mkanda katika muda wa saa 2, dakika 14 na sekunde 18.

Chepngetich amewashukuru mashabiki wake kwa pongezi zao kufuatia ushindi.

Ruth Chepng'etich
Ruth Chepng'etich
Image: HISANI

Bingwa wa mbio za Chicago Marathon Ruth Chepngetich amewashukuru mashabiki wake kwa pongezi zao kufuatia ushindi wake siku ya Jumapili.

Chepngetich alifanikiwa kutetea taji lake katika kinyang'anyiro hicho baada ya kuvunja mkanda katika muda wa saa 2, dakika 14 na sekunde 18.

“Nina furaha sana kwa matokeo bora siku ya Jumapili katika Benki ya Amerika ya Chicago Marathon, mbio ambazo nitazikumbuka daima! Asanteni nyote kwa ujumbe wenu mzuri. Nitachukua muda wangu kufurahia, kisha nirudi kazini. Mungu awabariki ninyi nyote,” Chepngetich alisema.

Chepngetich aliahidi kuvunja rekodi katika mbio zake zijazo.

"Nilitaka kuvunja rekodi ya dunia. Mwaka ujao niko tayari kurejea tena,” Chepngetich alisema.