Evans Chebet ashinda mbio za Boston marathon,huku Kipchoge akishikilia nafasi ya 6

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mbio za Boston Marathon.

Muhtasari
  • Mtanzania Gabriel Geay alivuka mstari wa mwisho kwa muda wa 02:06:04 na kuambulia fedha huku Benson Kipruto akiambulia nafasi ya tatu. Kipruto alirekodiwa 02:06:06.

Evans Chebet alifanikiwa kutetea taji lake la Boston Marathon mnamo Aprili 17, baada ya kutumia muda wa 2:05:54.

Geoffrey Mutai anashikilia rekodi ya kozi ya Boston Marathon ya 2:03:02 kutoka 2011.

Chebet alishinda taji hilo mwaka jana katika ukumbi huo huo.

Mtanzania Gabriel Geay alivuka mstari wa mwisho kwa muda wa 02:06:04 na kuambulia fedha huku Benson Kipruto akiambulia nafasi ya tatu. Kipruto alirekodiwa 02:06:06.

Mwanariadha nguli wa Kenya Eliud Kipchoge alishika nafasi ya 6.

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mbio za Boston Marathon.

Gwiji huyo wa mbio za masafa marefu  ameshinda rekodi ya London Marathon mara nne, huku pia akijivunia idadi sawa ya ushindi katika mbio za Berlin marathon.

Zawadi ya fedha taslimu ya mshindi kwa wanaume na wanawake imepangwa kuwa dola 150,000 ambazo ni sawa na Sh20 milioni.

Kwa mshindi wa Medali ya Fedha, ambayo ni nafasi ya pili, washindi watachukua hadi dola 75,000 sawa na Sh10 milioni.

Kwa Mechi ya Shaba, ambayo pia inatajwa kuwa mshindi wa pili, watakaoshikilia nafasi hiyo watajinyakulia dola 40,000 ambazo ni sawa na Sh5.2 milioni.