Mwanaridha wa Kenya anayeshikilia rekodi ya dunia asimamishwa kwa muda

Mnamo 2020 Rhonex Kipruto alivunja rekodi ya dunia ya mbio kilomita 10 huko Valencia.

Muhtasari

•Mwanariadha Rhonex Kipruto amesimamishwa kwa muda kwa madai ya ukiukaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Image: BBC

Mwanariadha wa Kenya anayeshikilia rekodi ya dunia amesimamishwa kwa muda kwa madai ya ukiukaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli, Kitengo cha Uadilifu cha Riadha (AIU) kinasema.

Mnamo 2020 Rhonex Kipruto alivunja rekodi ya dunia ya mbio kilomita 10 huko Valencia

Pia alishinda medali ya shaba kwenye Mashindano ya Dunia ya 2019 kwa utendaji wake katika mbio za mita 10,000.

Kesi itaamua hatima yake ya mwisho.