Ferdinand Omanyala amaliza wa pili katika mashindano ya Zagreb

Ferdinand Omanyala amaliza katioka nafasi ya pili kwenye mbio za mita 100, nyuma ya Courtney Lindsey,Zagreb.

Muhtasari

•Omanyala alimaliza katika nafasi ya pili katika mbio za mita 100, nyuma ya Lindsey Courtney aliyeshinda katika pambano hilo kwa mda wa sekunde 9.97.

•Omanyala sasa atabadilisha dhamira na kujiandaa kwa mashindano ya Wolrd Athletics Championship ambayo yataandaliwa Tokyo,Japan.

FERDINAND OMANYALA
Image: FACEBOOK

Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika ,kutoka taifa la Kenya Ferdinand Omanyala, alimaliza katika nafasi ya pili katika mbio za mita 100 kwenye mashindano ambayo yalikuwa yameandaliwa katika mji wa Zagreb taifa la Croatia.

Omanyala alimaliza katika nafasi ya pili lakini bado kuna matumaini kwake baada ya kuwa akiandikisha matokeo duni chini ya kipindi cha mwezi mmoja.

Lindsey Courtney kutoka Amerika alishinda mbio hizo kwa muda wa 9.97 mbele ya Omanyala aliyemaliza kwa sekunde 10.02.

Kwenye mbio hizo, Omanyala alianza kwa kasi ya chini lakini akajikaza na kupambana hadi kumaliza kattika nafasi hiyo ya pili.

Omanyala ndiye alikuwa bingwa mtetezi katika mbio hizo za Zagreb,baada ya kutwaa ushindi katika makala yaliyopita mwaka wa 2023.

Omanyala ambaye alikuwa anatafuta ushindi baada ya kufika fainali katika mashindano ya olimpiki, yaliyoandaliwa Ufaransa, alimaliza nafasi ya saba katika fainali hiyo.

Omanyala alimaliza katika nafasi ya saba kwenye katika mbio za Diamond League ambazo ziliandaliwa Rome. Mwanariadha Letsile Tebogo kutoka Botswana  akizoa ushindi.

Kwa sasa bado hayuko wazi kanakwamba atashiriki katika mashindano ya Fainali za Diamond League.Kwa sasa anashikilia katika nafasi ya 12 akiwa na pointi 9 ,na inahitajikana wanariadha nane wa kwanza katika mbio hizo.

Kwa sasa Omanyala atakuwa anazia pakubwa mbio za dunia hapo mwaka wa 2025, katika taifa la Japan hususan mji wa Tokyo.