Tanzia:Mwanakandanda Cristiano Ronaldo afiwa na mtoto wake

Muhtasari
  • Mwanakandanda Cristiano Ronaldo afiwa na mtoto wake
Mchezaji wa Man-U, Christiano Ronaldo
Mchezaji wa Man-U, Christiano Ronaldo
Image: Facebook

Cristiano Ronaldo ni mmoja wa wachezaji bora wa wakati wake na hii ameimarisha katika urithi kupitia michezo ambayo amecheza kwa miaka mingi kutokana na umri wake sasa.

Amepata watoto kadhaa na mtoto wake wa kwanza wa kiume ni mmoja wa wachezaji bora katika timu ya vijana ya Manchester United ambapo amefanya vyema katika maisha yake yote ya ujana.

Cristiano Ronaldo hivi karibuni alifunga mabao ambayo yamemfanya amwagiwe sifa nyingi lakini kwa sasa  yeye na Mpenzi wake Georgina wanaomboleza kifo cha mtoto wao.

Kupitia kwenye Mitandao ya Kijamii, Cristiano Ronaldo ametangaza kuwa amefiwa na mtoto wake wa kiume akiwa hospitalini.

Haijulikani kwa kina kuhusu jinsi mvulana huyo mdogo aliaga dunia lakini Cristiano anasema kwamba madaktari walijitahidi kuokoa maisha yake bila mafanikio.

"Ni kwa masikitiko yetu makubwa tunalazimika kutangaza kwamba mtoto wetu wa kiume ameaga dunia. Ni maumivu makubwa zaidi ambayo wazazi wowote wanaweza kuhisi. Kuzaliwa tu kwa mtoto wetu wa kike kunatupa nguvu ya kuishi wakati huu kwa matumaini na furaha,""Tungependa kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa huduma na usaidizi wao wote wa kitaalam. Sote tumehuzunishwa na tunaomba faragha katika wakati huu mgumu sana, Mtoto wetu wa kiume, wewe ni malaika wetu. Tutakupenda daima." - Imeeleza Taarifa ya @cristiano aliyoitoa kupitia Ukurasa wake wa Twitter.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.