Iker Casillas aomba msamaha kuhusu kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Ujumbe huo ulifutwa ndani ya saa moja.

Muhtasari

•Casillas alipokea jumbe nyingi za kumuunga mkono, akiwemo mchezaji mwenzake wa zamani wa Hispania Carles Puyol ambaye aliandika: "Ni wakati wa kusimulia hadithi yetu, Iker.

Iker Casillas
Image: BBC

Akaunti ya gwiji wa zamani wa Real Madrid na Hispania Iker Casillas iliandika kuhusu kwamba anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Hata hivyo muda mfupi uliopita, Iker amejitokeza na kuandika tena kwamba, akaunti yake ilidukuliwa, lakini sasa imerejea sawa akiomba msamaha kwa mashabiki na jamii ya wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

'ilidukuliwa akaunti. Bahati nzuri kila kitu kiko sawa sasa. Naomba radhi kwa washabiki wangu, na pia jamii ya wapenzi wa jinsia moja', aliandika Iker kwa lugha ya kihispania.

Kabla ya kuomba msamaha akaunti ya kipa huyo wa zamani aliyeshinda Kombe la Dunia akiwa na Hispania iliandika kwenye Twitter: "Natumai unaheshimu: mimi najihusisha na mapenzi ya jinsia moja."

Ujumbe huo ulifutwa ndani ya saa moja.

Haya yanajitokeza ikiwa ni mwaka mmoja tangu atengane na mtangazaji na mwanamitindo mstaafu Sara Carbonero mnamo Machi 2021 lakini akasema wataendelea kuwa karibu ili kuendeleza "kazi nzuri" ya kulea watoto wao wawili.

Baada ya akaunti hiyo kutangaza hivyo Casillas akaepokea ujumbe mwingi wa kumuunga mkono, akiwemo mchezaji mwenzake wa zamani wa Hispania Carles Puyol ambaye aliandika: "Ni wakati wa kusimulia hadithi yetu, Iker." Akiweka na emoji ya moyo na busu. Ujumbe ambao pia umeibua mjadala.

Ingawa baadaye Puyol alikosolewa ikionekana kufanya mzaha.

Mbali na Hispania, Real Madrid amewahi kuichezea Porto kwa misimu mitano mpaka mwaka 2020 alipotundika daruga kucheza soka la ushindani la kiwango cha juu.