BINGWA

Ronaldo amefunga mabao zaidi ya 700 kufikia sasa

Kwa miaka tisa aliyoichezea miamba ya Uhispania Real Madrid, alifunga mabao 450 katika mechi 438.

Muhtasari

•Ronaldo alitikisa nyavu mara 101 alipokuwa akiichezea Juventus na kufunga mabao mengine matano akivalia jezi ya Sporting Lisbon, Ureno.

•Bao lake dhidi ya Everton - likiwa la pili msimu huu - linamaanisha kuwa sasa ameifungia Manchester United jumla ya mabao 144 katika mechi 340 alizocheza na klabu hiyo.

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo
Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo
Image: HISANI

Mshambulizi wa Manchester United Cristiano Ronaldo ameandika ukurasa mpya katika historia baada ya kufunga bao lake la 700 katika soka la vilabu.

Ronaldo, 37, alionyesha umahiri wake baada ya kucheka na wavu dakika ya 44 na kuipa Manchester United ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton katika pambano lao la Ligi Kuu ya Uingereza Uwanja wa Goodison Park Jumapili.

Bao lake dhidi ya Everton - likiwa la pili msimu huu - linamaanisha kuwa sasa ameifungia Manchester United jumla ya mabao 144 katika mechi 340 alizocheza na klabu hiyo.

Kwa miaka tisa aliyoichezea miamba ya Uhispania Real Madrid, alifunga mabao 450 katika mechi 438.

Ronaldo alitikisa nyavu mara 101 alipokuwa akiichezea Juventus na kufunga mabao mengine matano akivalia jezi ya Sporting Lisbon, Ureno.

Alifunga mabao 51 katika vikombe vya nyumbani, yakiwemo Copa del Rey (22), FA Cup (13), Spanish Super Cup, EFL Cup, Coppa Italia (manne kila moja), Taca de Portugal na Supercoppa Italy (zote.)

Alikusanya tisa zaidi kwenye Kombe la Dunia la Klabu (saba) na UEFA Super Cup (mbili). Yote hayo yanaongeza hadi mechi 945 za klabu kubwa na mabao 700.