Didier Drogba azungumzia madai ya kubadili dini kuwa Muislamu

Raia huyo wa Ivory Coast pia alidokeza kuwa anavutiwa na baraka za Uislamu.

Muhtasari

•Picha za Drogba akikutana na kundi la Waislamu na kusali nao zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa kuwa amechukua hatua ya kujiunga na dini hiyo.

•Mshambulizi huyo wa zamani wa Chelsea amesema alikuwa anaonyesha heshima kwa marafiki zake Waislamu ambao alitembelea.

katika mkutano na kundi la Waislamu
Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba katika mkutano na kundi la Waislamu
Image: HISANI

Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba amepuuzilia mbali madai kuwa amebadili dini.

Siku za Jumatatu, picha za nahodha huyo wa zamani wa Ivory Coast akikutana na kundi la Waislamu na kusali nao zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa kuwa amechukua hatua ya kujiunga na dini hiyo.

Drogba hata hivyo ameeleza kwamba alikuwa anaonyesha heshima kwa marafiki zake Waislamu ambao alitembelea.

"Hadithi hii inasambaa sana, lakini sijabadilisha dini. Nilikuwa tu nikitoa heshima kwa ndugu zangu Waislamu niliokuwa nimewatembelea kijijini. Muda wa umoja. Upendo mwingi na baraka kwa wote," Drogba alijibu kupitia akaunti yake ya Twitter.

Raia huyo wa Ivory Coast alidokeza kuwa pia anavutiwa na baraka za Uislamu.

Picha za mwanasoka huyo wa zamani akikutana na kundi hilo la Waislamu zilizua mjadala mkali miongoni mwa wapenzi wa dini na kandanda kwenye mitandao ya kijamii. Wanamitandao wengi Waislamu walifurahi kumkaribisha kwenye dini hiyo huku baadhi ya wanamitandao wengine wakihisi haikuwa hatua nzuri.

Takriban miezi mitano iliyopita, kiungo wa Arsenal Thomas Partey alibadili jina na kuwa Yakubu baada ya kubadili dini na kuwa Muislamu kufuatia ndoa yake ya  na kipusa Mmorocco, Sara Bella.

Hata hivyo, licha ya jina lake kubadilishwa, kiungo huyo matata bado anatambuliwa kama Partey wakati akiichezea Wanabunduki.

Isitoshe, jezi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 bado inaandikwa Thomas kwenye sehemu ya nyuma ya anapocheza