Kombe la Dunia Qatar 2022: Ukweli kuhusu Sadio Mané

Tangu akiwa na umri mdogo alitamani kuwa mchezaji soka.

Image: BBC

Sadio Mane mwenye umri wa miaka 30, ni mmoja wa wachezaji bora zaidi wa soka duniani kwa sasa. Huku akijiandaa kuiwakilisha nchi yake Senegal katika Kombe la Dunia la Qatar 2022, huu ndio ukweli kumhusu.

  • Mané mwenye alizaliwa katika kijiji cha Bambali, Sédhiou, nchini Senegal
  • Tangu akiwa na umri mdogo alitamani kuwa mchezaji soka
  • Baba yake yake ambaye alikuwa Iman alimzuia kucheza soka alipokuwa mtoto
  • Lakini akiwa na umri wa miaka saba, baba yake alifariki na alipotimiza umri wa miaka 15, alitoroka kijijini kwao kwenda katika mji mkuu Dakar kutekeleza azma yake ya kuwa mwanasoka.
  • Mwaka 2009, wakati alipokuwa akichezea timu ya M’Bour ligunduliwa na maskauti na baadaye alitambuliwa na Génération Foot,
  • Mwaka 2011 alijiunga na klabu ya Metz, ambayo ilikuwa na ushirika na Génération Foot
  • Alijiunga na klabu ya Austria ya Salzburg tarehe 31 Agosti 2012
  • Baadaye alijiunga na klabu ya Southampton na kuichezea katika msimu wa mwaka 2014- 2015
  • Mwaka 2016 hadi 2022 aliichezea klabu ya Liverpool lakini tarehe 22 June, 2022 alijiunga na klabu ya Ligi ya ujerumani Bundesliga, Buyern Munich.