Ramos akutana na Salah, miaka 5 tangu kumsababishia jeraha la bega

Katika faniali za mwaka 2018 baina ya Real Madrid na Liverpool, beki huyo alimvuruta Salah mkono na kumuangusha chini, kusababisha kuondolewa mchezoni.

Muhtasari

• Salah aliingia chumbani, na yeye na Ramos wakakumbatiana kwa tabasamu kabla ya kuanza kumsalimia nyota wengine.

Ramos hatimaye akutana na Salah
Ramos hatimaye akutana na Salah
Image: Mirror

Baada ya miaka mitano tangu kukutana kwao kwenye fainali za klabu bingwa barani Ulaya, hatimaye mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa la Misri, Mohammed Salah na beki wa PSG na timu ya taifa ya Uhispania wamekutana na kusalimiana.

Wawili hao walikutana katika tamasha la kuwazawidi wachezaji waliofana lililoandaliwa Dubai mapema wiki hii na kwa mara ya kwanza tangu tukio la kuumia kwa Salah baada ya kutegwa na Ramos, wawili hao walisalimiana kwa furaha.

Katika pambano hilo la fainali lililowakutanisha Real Madrid na Liverpool, Ramos alituhumiwa kumjeruhi bega Salah, jambo ambalo lilimlazimu kutoka nje ya mchezo, na kuwashuhudia Wekundu hao wakichapwa mabao 3-1 na Real Madrid.

Wachezaji hao wawili hawajakutana uwanjani tangu tukio hilo la mjini Kyiv, Ukraine. Nyota huyo wa PSG hakucheza robo fainali dhidi ya Reds na alihamia PSG wakati Liverpool ilipocheza na Madrid katika fainali msimu uliopita.

Salah aliingia chumbani, na yeye na Ramos wakakumbatiana kwa tabasamu kabla ya kuanza kumsalimia nyota wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic. Hakukuwa na dalili yoyote ya uhasama kati ya wachezaji hao wawili lakini kwa kuangalia nyuma mwingiliano lazima ulikuwa wa shida kidogo, kulingana na jarida la The Sun.

Mwaka jana kabla ya pambano la Real Madrid na Liverpool kwenye fainali za klabu bingwa barani, Salah alinukuliwa na jarida la Reuters akisimulia kumbukumbu za fainali ya 2018 na kusema kwamab jeraha alilosababishiwa na Ramos lilikuwa moja la kumuumiza moyo sana baada ya kulazimika kuondoka uwanjani kunako dakika ya 30.