Cristiano Ronaldo kuondoka Manchester United mara moja

"Klabu inamshukuru kwa mchango wake mkubwa katika misimu miwili Old Trafford," ilisema taarifa ya Manchester United.

Muhtasari
  • Uamuzi huo unafuatia mahojiano yenye utata ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliikosoa klabu hiyo na kusema "hana heshima" kwa meneja Erik ten Hag
Amefichua kuwa hana raha katika klabu hiyo ya Premier league.
Mshambulizi wa Manchester United Christiano Ronaldo. Amefichua kuwa hana raha katika klabu hiyo ya Premier league.
Image: GETTY IMAGES

Mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuondoka Manchester United mara moja.

Uamuzi huo unafuatia mahojiano yenye utata ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliikosoa klabu hiyo na kusema "hana heshima" kwa meneja Erik ten Hag.

Pande zote mbili zilisema kwamba kuondoka kwa Ronaldo "ni uamuzi uliokubaliwa kwa pamoja".

"Klabu inamshukuru kwa mchango wake mkubwa katika misimu miwili Old Trafford," ilisema taarifa ya Manchester United.

Walimtakia "yeye na familia yake heri kwa siku zijazo" na wakaongeza "kila mtu katika Manchester United anabakia kulenga kuendeleza maendeleo ya timu chini ya Erik ten Hag na kufanya kazi pamoja kuleta mafanikio uwanjani".

Ronaldo yuko pamoja na Ureno kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar na anatazamiwa kuwa nahodha wao katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi H dhidi ya Ghana Alhamisi.

"Kufuatia mazungumzo na Manchester United tumekubaliana kwa pamoja kumaliza mkataba wetu mapema," ilisema taarifa ya fowadi huyo.