Mykhailo Mudryk: Shakhtar waahidi kutoa £22m kwa vita vya Ukraine baada ya uhamisho wa Chelsea

Ukraine ilivamiwa na Urusi mwaka wa 2022.

Muhtasari

•Chelsea ilimsajili Mudryk kutoka Shakhtar siku ya Jumapili kwa mkataba wa thamani ya hadi £89m.

•Akhmetov alisema alikuwa na "hisia mseto" kuhusu Mudryk, 22, kuondoka Shakhtar kwenda Chelsea.

Mykhailo Mudryk
Image: BBC

Rais wa Shakhtar Donetsk Rinat Akhmetov ameahidi kutoa pauni milioni 22 kwa juhudi za vita vya Ukraine kufuatia uhamisho wa Mykhailo Mudryk kwenda Chelsea.

Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza ilimsajili Mudryk kutoka Shakhtar siku ya Jumapili kwa mkataba wa thamani ya hadi £89m, rekodi ya uhamisho kwa soka ya Ukraine.

Akhmetov alisema pesa hizo zitasaidia mradi uliopewa jina la 'Moyo wa Azovstal,' unaolenga "kusaidia watetezi wa Mariupol na familia za wanajeshi walioangamia".

Ukraine ilivamiwa na Urusi mnamo 2022.

"Nataka kushukuru ulimwengu mzima uliostaarabika kwa kuisaidia Ukraine," alisema Akhmetov.

"Leo tunaweza kuzungumza kuhusu soka la Kiukreni shukrani kwa jeshi la Ukraine, watu wa Ukraine, na msaada mkubwa wa ulimwengu mzima uliostaarabu."

Akhmetov alisema alikuwa na "hisia mseto" kuhusu Mudryk, 22, kuondoka Shakhtar kwenda Chelsea.

"Sijawahi kufanya siri kuwa ndoto yangu ni kushinda mataji ya Uropa," alisema.

"Hii ina maana kwamba wachezaji kama Mudryk wanapaswa kualikwa kwenye klabu yetu, kwenye michuano yetu ya Ukraine, na tunapaswa kushinda mataji ya Ulaya na wachezaji kama hao.