Historia mbaya ya Man City kwenye uwanja wa Tottenham Hotspurs

Vijana wa Pep Guardiola walipoteza 1-0 kwa wachezaji 10 wa Spurs.

Muhtasari

•Katika mchuano wa mwisho, siku ya Jumapili jioni, vijana wa Pep Guardiola walipoteza 1-0 kwa wachezaji 10 wa Spurs.

•City hawajakosa tu kushinda, bali pia hawajafunga bao lolote katika mechi 5  zilizopita kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur.

Mchezaji wa Man City, Erling Halaand
Image: HISANI

Mabingwa wa EPL  msimu 2021/22, Manchester City wameshindwa kushinda mechi yoyote katika uwanja mpya wa Tottenham Hotspurs tangu klabu hiyo yenye maskani yake London ilipohama takriban miaka 4 iliyopita.

Tottenham Hotspur walihamia rasmi kwenye uwanja mpya wa Tottenham Hotspur Stadium  mnamo Aprili 3, 2019 baada ya ukarabati kukamilika na tangu wakati huo wameikaribisha Man City huko mara tano.

City hawajakosa tu kushinda, bali pia hawajafunga bao lolote katika mechi 5  zilizopita kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur.

Katika mchuano wa mwisho, siku ya Jumapili jioni, vijana wa Pep Guardiola walipoteza 1-0 kwa wachezaji 10 wa Spurs.

Bao la pekee la mshambulizi Harry Kane katika dakika ya 15 liliwapatia ushindi Tottenham na kuwaweka katika nafasi bora ya kupigania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa katika msimu ujao.

Tottenham walionyesha ubabe katika mechi hiyo lakini mambo yalikuwa makali dakika za mwisho baada ya beki Christian Romero kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 87 kwa kumchezea vibaya Jack Grealish.

Klabu hiyo ya London Kaskazini pia ilikosa huduma za Kocha wao mkuu Antonio Conte ambaye alifanyiwa upasuaji wa kibofu cha nyongo Jumatano wiki iliyopita.

Wiki jana, klabu hiyo ilifichua kwamba Conte hivi majuzi alikumbwa na maumivu makali ya tumbo ambayo yalimlazimu kutafuta huduma za matibabu.

Baada ya vipimo kadhaa, ilipendekezwa afanyiwe upasuaji wa kuondoa kibofu cha nyongo na anatarajiwa kufanyiwa utaratibu huo hivi leo, Februari 1.

"Antonio Conte hivi majuzi aliugua kwa maumivu makali ya tumbo. Kufuatia kugundulika kwa ugonjwa wa cholecystitis, atafanyiwa upasuaji wa kuondoa kibofu cha nyongo leo na atarejea kufuatia muda wa kupona," Taarifa ya Tottenham ilisoma.

Spurs walimtakia mkufunzi huyo afueni ya haraka huku wakitazamia kurejea kwake ili awaongoze katika kuwinda taji la EPL.