Manchester City kufukuzwa kutoka kushiriki ligi kuu ya EPL kwa ukiukaji wa kanuni za usajili

Mashtaka hayo yanahusiana na ukiukaji wa kanuni kwa misimu tisa kati ya 2009 na 2018.

Muhtasari

• Uchunguzi kuhusu mahusiano ya klabu hiyo umedumu kwa miaka minne.

Timu ya City watiwa kwenye supu
Timu ya City watiwa kwenye supu
Image: Twitter

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya EPL, Manchester City huenda wakafukuzwa kutoka kushiriki ligi kuu ya EPL baada ya kupatikana na makosa zaidi ya 100 ya kukiuka masharti ya uhamisho wa wachezaji kwa muda mrefu.

Uchunguzi kuhusu mahusiano ya klabu hiyo umedumu kwa miaka minne.

Na sasa Premier League wamechapisha matokeo yao kwenye tovuti yao na haitumi taarifa nzuri kwa klabu ya Etihad.

Ingawa kwa wakati huu wameshtakiwa lakini hawajapatikana na hatia - lakini City hawataweza kukata rufaa kwa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ikiwa uamuzi huo utapitishwa..

Mashtaka hayo yanahusiana na ukiukaji wa kanuni kwa misimu tisa kati ya 2009 na 2018, huku uchunguzi ukianza Desemba 2018.

Hilo lilichochewa kufuatia uchapishaji wa nyaraka zilizovuja na tovuti ya Ujerumani Der Spiegel - huku uchunguzi ukilenga maeneo matatu mahususi.

Kulingana na jarida la The Sun, Suala la kwanza linalodaiwa ni "wachezaji wa umri wa chini walishinikizwa kusaini mikataba na City kupitia malipo ya pesa".

Pili, kwamba wafadhili wa Abu Dhabi "walitoa sehemu tu ya malipo yao kwa klabu", huku mmiliki Sheikh Mansour akipinga iliyobaki, na kuzidisha mapato ya udhamini.

Mwishowe, bosi wa zamani Roberto Mancini alipokea "sehemu kubwa" ya fidia kutoka kwa "mkataba wa uwongo wa ushauri" alipoondoka katika kilabu mnamo 2013.

Pia inadaiwa na Ligi Kuu ya Uingereza katika matokeo yao ambayo hayajawahi kushuhudiwa kuwa City haikufuata kanuni za Uefa zinazohusu utoaji wa leseni za klabu na uchezaji wa haki za kifedha mnamo 2013-14 na kati ya 2014-15 na 2017-18.