Mkwasi wa Qatar kuinunua Manchester United kwa kitita kinono cha pesa

“Hiyo ni pamoja na kumpa Ten Hag kipaumbele kwa uhamisho ili kumruhusu kushindania kusajili vipaji asili"

Muhtasari

• Utwaaji huo huenda ukapata pingamizi kutokana na rekod mbaya ya haki za kibinadamu kutoka kwa taifa hilo la Uarabu.

Image: MANUTD.COM

Miezi michache iliyopita, wamiliki wa klabu ya soka ya Manchester United kutoka Marekani wanaojulikana kama familia ya Glaziers waliweka taarifa wazi kwamba walikuwa wanatathmni hatua ya kuuza klabu hiyo.

Imebainika kwamba sasa kuna timu ya raia matajiri wa pesa za mafuta kutoka taifa la Qatar ambao wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuinunua timu hiyo.

Kulingana na jarida la Mail, Vyanzo vya habari vimefichua kundi la watu binafsi, matajiri wa juu wanaoishi katika jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, linalochochewa na uenyeji wa Qatar wa Kombe la Dunia, wameelekeza macho yao kwenye klabu wanayoiona kama 'vito vya taji la soka'.

Watatoa ofa kwa United katika siku zijazo, kabla ya muda wa mwisho wa mwezi wa Februari uliowekwa na Glazers, na wana imani kwamba ombi lao litaondoa ushindani.

Jarida hilo lilisema kuwa matajiri hao pia wanalenga kutoa kitika kimono kwa kocha mkuu Eric Ten Hag ili kufanya usajili wa maana kwenye timu na kuimarisha ushindani wa kuwania mataji ndani ya nje ya Uingereza.

“Hiyo ni pamoja na kumpa Ten Hag kipaumbele kwa uhamisho ili kumruhusu kushindania kusajili vipaji kujiunga na klabu tajiri zaidi duniani.”

Kikwazo kimoja kinachowezekana ni umiliki wa Qatar Sports Investments wa Paris Saint-Germain. Kulingana na sharia za FIFA, Kampuni au Chombo kimoja hakiwezi kumiliki vilabu viwili kwenye shindano moja - na United na PSG zinaweza kukutana kwenye mashindano ya Ulaya.

Utwaaji huo utahitaji kuidhinishwa na Ligi Kuu na huenda ukakabiliwa na upinzani katika baadhi ya maeneo, ikizingatiwa wasiwasi juu ya rekodi ya haki za binadamu kwenye taifa hilo la Uarabuni.