Aboubakar: Ronaldo alijaribu kunizuia nisiondoke klabu ya Saudi

"Na aliniambia ni bora, ikiwa familia iko mbali sana, ni ngumu zaidi.

Muhtasari
  • Licha ya nyota huyo wa zamani wa Man United na Real Madrid kujaribu kumzuia kuondoka, Aboubakar aliamua kurejea Besiktas ya Uturuki
Nahodha wa Cameroon Vincent Aboubakar
Image: BBC

Nahodha wa Cameroon Vincent Aboubakar amesema Cristiano Ronaldo alijaribu kuzungumza naye ili aachane na Al Nassr, baada ya nyota huyo wa Ureno kuwasili katika klabu hiyo ya Saudia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye alikuwa amebaki na miezi sita katika mkataba wake wa Al Nassr, alijua kabisa kwamba mchezaji wa kigeni angelazimika kutolewa kwa ajili ya mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or.

Licha ya nyota huyo wa zamani wa Man United na Real Madrid kujaribu kumzuia kuondoka, Aboubakar aliamua kurejea Besiktas ya Uturuki kwa kusaini miaka miwili na nusu mnamo mwezi Januari.

"Tulizungumza kidogo na Cristiano aliniambia kwamba ni vyema nibaki ila nilimwambia hapana, na kwamba nitaondoka kwa sababu za kifamilia," Aboubakar aliiambia Talents d'Afrique kwenye Canal+.

“Aliniuliza familia yangu iko wapi, nikamwambia iko Ufaransa lakini napendelea kwenda Uturuki, ni karibu zaidi.

"Na aliniambia ni bora, ikiwa familia iko mbali sana, ni ngumu zaidi.

Kwa kuwa nilikuwa nataka kuondoka tu."