Klabu ya soka yapigwa faini kwa kosa la afisa wake kukojoa uwanjani

Klabu ya Nigeria imetozwa karibu $1,000 (£900) baada ya afisa mmoja kupigwa picha akikojoa uwanjani.

Muhtasari

•Picha hiyo iliyopigwa kabla ya mchezo wa nyumbani wa Shooting Stars dhidi ya Akwa United Jumapili, ilisambaa.

Image: HISANI

Chama cha kandanda cha Nigeria kimeitoza faini klabu ya daraja la kwanza huko Ibadan ya karibu $1,000 (£900) baada ya afisa mmoja kupigwa picha akikojoa uwanjani.

Picha hiyo iliyopigwa kabla ya mchezo wa nyumbani wa Shooting Stars dhidi ya Akwa United Jumapili, ilisambaa.

Afisa huyo, Auwal Mohammed, pia amesimamishwa kwa mwaka mmoja kujihusisha na shughuli zozote zinazohusiana na Ligi ya Soka ya Kulipwa ya Nigeria (NPFL).

Katika barua kwa Shooting Stars kutoka kwa Kamati ya Usimamizi ya Muda, chombo kinachosimamia NPFL, ilielezea tukio hilo kama "kitendo cha kuchukiza" ambacho kilileta sifa mbaya.

"Ulishindwa kudhibiti mienendo ya maafisa wako ambayo ilisababisha Bw Auwal Mohammed kukojoa uwanjani Umma ukishuhudia," ilisema sehemu ya barua hiyo.