CR7 akanusha kushiriki madai ya mapenzi na mwanablogu wa Venezuela mwaka 2022

Mwanamitindo huyo alisema kwamba Ronaldo alimwalika kwenye chumba cha hoteli na katika mazungumzo akajikuta ameshiriki kitendo naye.

Muhtasari

• Mwanamitindo huyo alisema kitendo hicho kilikuwa kwa makubaliano lakini anahisi alirubuniwa na umaarufu wa Ronaldo.

christinao Ronaldo akanusha kushiriki mapenzi na mwanamitindo wa Venezuela
christinao Ronaldo akanusha kushiriki mapenzi na mwanamitindo wa Venezuela
Image: Instagram

Nyota wa Al-Nassr Cristiano Ronaldo amekanusha vikali madai ya kumsaliti mpenzi wake Georgina Rodriguez baada ya vyombo vya habari vya Ureno kuripoti kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanablogu wa Venezuela Georgilaya.

Georgilaya alidai kuwa tukio hilo lilitokea mwaka jana Machi 25, 2022, wakati kikosi cha Ureno (nahodha wa Cristiano Ronaldo) kikijiandaa na Kombe la Dunia la FIFA 2022.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United inasemekana alitumia usiku kucha na Georgilaya katika hoteli ya Solverde huko Vila Nova de Gaia, kaskazini mwa Ureno, katika chumba namba 312. Georgilaya anadai kuwa Ronaldo alimtumia ujumbe wa kumualika chumbani kwake baada ya kupiga picha za selfie naye na wachezaji wengine wa soka. Aliandika kwenye Instagram, kulingana na The Sun.

“Nilipoisoma ile meseji nilidhani nikienda huko tutazungumza tu, tufahamiane vizuri, labda nipate picha nyingine, sikufikiria kuwa katika hali hiyo kungekuwa na mapenzi. Ukweli ni kwamba, ilitokea. Ilikubaliwa kwa upande wangu, lakini licha ya hilo, nilihisi kudanganywa, na umaarufu na nguvu ya Cristiano Ronaldo,” mwanamitindo huyo alisema.

Georgilaya anadai kuteswa na hatia ya uchumba huo, kutokana na kumdanganya mumewe kwa kulala na Cristiano Ronaldo. Pia hataki 'umaarufu au pesa' na amefichua jumbe za maandishi kutoka kwa Ronaldo na marafiki zake, akiwemo Jose Semedo.

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or alikanusha upesi tuhuma hizo baada ya habari hiyo kuchapishwa kwenye gazeti la Correio da Manhã nchini Ureno. Msemaji wake alisema:

"Huu ni uwongo kabisa na udhalilishaji."

Familia ya Ronaldo itakuwa na matumaini kwamba hizi ni tuhuma za kutafuta umakini. Gwiji huyo wa Real Madrid amekuwa akichumbiana na mpenzi wake wa sasa Georgina Rodriguez tangu 2016 walipokutana kwenye duka la Gucci mjini Madrid.

Georgina Rodriguez kwa sasa ni mwanamitindo na ana watoto watatu wa kibaolojia na watoto watatu wa kambo na Ronaldo.

Wanandoa hao walihamia Saudi Arabia Januari 2023 kufuatia Mreno huyo kuhamia klabu ya Saudi Pro League ya Al-Nassr kwa mkataba wa miaka miwili. Uhamisho wao ulivutia wakati Ronaldo na Georgina Rodriguez walipotofautiana na sheria inayosema kwamba watu wasiofunga ndoa hawaruhusiwi kuishi pamoja.