`Bruno fernandes hafai kuwa nahodha wa Man United`

"Kuna watu ambao wamehitimu zaidi kuwa nahodha," Sutton alisema.

Muhtasari

•Bruno Fernandes alikosolewa kwa tabia na mtazamo wake katika mchuano wa United dhidi ya Liverpool Jumapili.

•Bruno alionekana kumsukuma msaidizi wa mwamuzi katika dakika ya 81. 

Image: BBC

Bruno Fernandes hapaswi kuwa nahodha wa Manchester United tena kufuatia kipigo cha aibu cha 7-0 Jumapili kutoka kwa Liverpool, kwa mujibu wa Chris Sutton.

Mreno huyo, ambaye anaongoza timu hiyo kama kaimu wa nafasi ya nahodha wa klabu hiyo Harry Maguire, alikosolewa kwa tabia na mtazamo wake katika mchezo huo.

"Kuna watu ambao wamehitimu zaidi kuwa nahodha," Sutton alisema.

"Fernandes sio kiongozi wao bora. Kuna wagombeaji wanaofaa zaidi yake, Casemiro akiwa mmoja."

Akiongea kwenye Klabu ya BBC 5 Live ya Jumatatu usiku , mshambuliaji huyo wa zamani wa ligi ya Premier Sutton, ambaye pia alimpendekeza Raphael Varane kama chaguo jingine, aliongeza: "Nadhani hapaswi kamwe kuwa nahodha tena wa Manchester United."

Pia alionekana kumsukuma msaidizi wa mwamuzi katika dakika ya 81. Hakuna hatua iliyochukuliwa na mwamuzi wakati huo na tukio hilo halichunguzwi na Chama cha Soka

BBC Sport pia imeambiwa kwamba hakuomba kubadilishwa hadi mwisho wa mechi, baada ya maswali kuulizwa kuhusu ishara alizoonesha kwenye benchi.

Wakati fulani, wakati Stefan Bajcetic wa Liverpool alipompita na mpira karibu na mstari wa nje wa uwanja , Fernandes alisimama badala ya kumfukuza kiungo huyo.

"Huo ulikuwa wakati mzuri sana jana," aliongeza Sutton.

"Hata licha ya kwamba hivyo United ilikuwa hali mbaya, huwezi tu kuruhusu mtu akupite kwa urahisi na ukate tamaa. Hivyo ndivyo nahodha wa Manchester United alifanya - na hiyo ni sura mbaya.

"Sidhani kama atalalamika ikiwa atavuliwa unahodha," aliongeza. "Nadhani siku za Bruno lazima zihesabiwe."

Kipigo hicho kilikuja siku saba baada ya Manchester United kushinda Kombe la Carabao - kombe lao la kwanza tangu kuwasili kwa Erik Ten Hag kama meneja Mei mwaka jana.

Wameshika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Premia na wametinga robo fainali ya Kombe la FA, pamoja na hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa.

Ten Hag, ambaye alielezea uchezaji wa timu yake dhidi ya wapinzani wao Liverpool kama "usio wa kitaalamu", alimuondoa kwenye fomu Marcus Rashford mwanzoni mwa msimu huu baada ya mshambuliaji huyo kukosa kukutana na timu, huku mkataba wa Cristiano Ronaldo ukikatizwa kwa makubaliano mwezi Novemba.

"Jinsi Ten Hag alivyoshughulika na Rashford, Ronaldo, ni hali ambayo anahitaji kuidhibiti," aliongeza Sutton. "Hag hana chaguo ila kumjulisha nani ni bosi wake."

Kuhusu unahodha wa United, mwandishi wa habari wa soka Rory Smith alisema: "Fernandes ni mpiganaji, ana mawazo ya kushinda kwa gharama yoyote. Kwangu mimi anaonekana mnyonge na mchoyo, lakini labda kwa wachezaji wengine wanaona hivyo kwa vile anatamani sana kushinda. "

Smith aliongeza: "Kama vile Bruno alivyokuwa na mapungufu mkubwa jana, ningeuliza ni nini kilichotokea kwa Casemiro na pia mabadiliko ya Ten Hag. Kulikuwa na mapungufu mengi zaidi hapo jana Zaidi ya Bruno Fernandes pekee."