Dele Alli aonekana na vidosho 4 kitandani akila starehe, pombe na dawa za kulevya

Vyanzo vya habari vilidai kwamba mchezaji huyo viwango vyake viliporomoka alitumia takribani shilingi milioni moja kwenye vinywaji vya pombe.

Muhtasari

• Vyanzo vilidai kuwa Dele analipwa £110,000 kwa wiki.

• Jarida la The Sun liliripoti kwamba Alli akiwa nchini Uturuki, alikula raha na starehe kwenye kilabu mara mbili chini ya siku 10

Dele Alli aonekana na wanawake 4 kitandani
Dele Alli aonekana na wanawake 4 kitandani
Image: Twitter

Picha ya Nyota wa Uingereza aliyeanguka, Dele Alli akijilaza kitandani na wasichana wanne na marafiki watatu wa kiume wakati wa tafrija ya usiku imezua gumzo mitandaoni.

Mchezaji huyo wa Everton ambaye yupo mkoponi Besiktas ya Uturuki alikuwa akijivinjari na wasichana wane wakiwa wamemzingira kitandani huku ikiripotiwa kuwa alitumia Zaidi ya £ 6,000 sawa na shilingi elfu 987 kwenye pombe kali aina ya champagne na tequila.

Ilikuwa ni usiku huohuo baadaye alipigwa picha akiwa na puto mdomoni na mitungi ya gesi inayomfanya mtu kuhisi kucheka, jambo ambalo lilisababisha wasiwasi kuonyeshwa juu yake katika ulimwengu wa soka.

Picha za kipekee zinaonyesha Dele, 27, akificha uso wake akiwa kitandani na wenzi wake akiwemo mchezaji wa zamani wa Chelsea Izzy Jay Brown, 26, na wasichana wanne baada ya safari ya Chinawhite jijini Manchester.

Jarida la The Sun liliripoti kwamba Alli akiwa nchini Uturuki, alikula raha na starehe kwenye kilabu mara mbili chini ya siku 10, ambapo alikuwa kwa mkopo Besiktas kutoka klabu ya sasa ya Everton.

Vyanzo vilidai kuwa Dele anayelipwa £110,000 kwa wiki, katika uhusiano na mwanamitindo wa Sports Illustrated Cindy Kimberly, 24, alimwacha Chinawhite na wasichana hao - angalau mmoja wao anasemekana kufanya kazi huko - saa 4 asubuhi.

Dele aliyewahi kuwa mchezaji bora wa soka wa England, alirejea Everton kwa matibabu ya majeraha ya nyonga baada ya kushindwa kwa mkopo nchini Uturuki.

Chanzo kimoja kilisema: "Dele alikuwa na wakati mzuri wa kunywa na wenzake kwenye kilabu.