CR7 huenda wakatengana na mkewe kwa sababu ya kutofautiana na mama ya mchezaji huyo

Majarida kadhaa kutoka Ureno yanadai kwamba mke wa Ronaldo Gerogina Rodriguez hana uhusiano mwema na mamake Ronaldo na hilo huenda litalemaza ndoa yao.

Muhtasari

• "Georgina hutumia siku yake katika duka la jumla huko Riyadh, na hiyo ndiyo sababu mojawapo kwa nini Cristiano hafurahishwi" - mwandishi wa bahari alidokeza.

Ronaldo na Mkewe katika hafla ya siku yake ya kuzaliwa
Image: Christiano Ronaldo (Facebook)

Nyota wa kandanda Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez kwa mara nyingine tena wako katikati ya uvumi kwamba kuna mvutano unaoongezeka katika uhusiano wao.

Uvumi huo uliibuka katika kipindi cha mazungumzo cha kituo cha runinga cha CMTV cha Ureno Noite das Estrelas, ambapo mwandishi wa habari Quintino Aires, rafiki wa karibu wa mama wa Ronaldo, alidai kuwa tabia za mwanasoka huyo zilionyesha kwamba hakuwa na furaha katika maisha yake ya kibinafsi.

"Haishi wakati wa furaha, na kadiri anavyosonga mbali na mama yake, ndivyo anavyopungua. Na sote tunajua kwa nini anazidi kuwa mbali na familia yake,” Aires alisema, akimnyooshea kidole mpenzi wa Ronaldo, Georgina Rodriguez.

"Georgina hutumia siku yake katika duka la jumla huko Riyadh, na hiyo ndiyo sababu mojawapo kwa nini Cristiano hafurahishwi na hadithi hii," aliongeza.

Maoni ya Aires yanakuja baada ya uvumi wa hapo awali mapema mwaka huu, kupendekeza mgogoro unaowezekana kati ya wanandoa hao. Hata hivyo, Georgina Rodriguez alikanusha uvumi huo kupitia akaunti yake ya Instagram, aki-share picha na Ronaldo kuonyesha uhusiano wao ni sawa na siku zote.

"Kuna mambo mengi mazuri yaliyosalia kuishi," Georgina alinukuu picha hiyo kwenye hadithi yake ya Instagram.

Licha ya kukanusha, mwandishi wa habari Leo Caeiro, ambaye pia anaonekana kwenye Noite das Estrelas, aliunga mkono maoni ya Aires kuhusu kutokuwa na furaha kwa Ronaldo katika uhusiano wake, akisema:

"Nimekuwa nikisema kwa miezi. Hawako vizuri na wana uwezekano wa kutengana. Ukweli ni kwamba Cristiano amechoshwa nayo.”

Mfululizo wa hivi majuzi wa kipindi cha hivi karibuni cha Georgina cha hali halisi ya TV, 'Mimi ni Georgina' Msimu wa 2, pia ulifichua mtindo wa maisha wa kigeni wa mshawishi huyo na shauku ya ununuzi wa kifahari, ambayo inaweza kuchangia uvumi wa mgawanyiko kati ya wanandoa hao.