Man U na Newcastle mbioni kumsajili Sadio Mane

Manchester United wanakamilisha mipango yao ya uhamisho wa majira ya kiangazi.

Muhtasari

• Manchester City wana nia ya kumsajili beki wa RB Leipzig na Croatia Josko Gvardiol.

• Kiungo wa kati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 27, anasakwa na AC Milan ambao.

Sadio Mane
Sadio Mane
Image: BBC

Manchester United na Newcastle United zimeibuka kuwa klabu zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kumsajili fowadi wa Bayern Munich na Senegal Sadio Mane, 31, kufuatia msimu mbaya wa kwanza nchini Ujerumani. (Mail)

Chelsea, Manchester United, Tottenham na Fulham ni miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji mshambuliaji wa Gent mwenye umri wa miaka 20 kutoka Nigeria Gift Orban. (Evening Standard)

Manchester United wanakamilisha mipango yao ya uhamisho wa majira ya kiangazi, huku kiungo wa kati wa Juventus Mfaransa Adrien Rabiot, 28, akirejea kwenye orodha yao walioteuliwa pamoja na mlinzi wa Napoli wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26. (Mirror).

Pamoja na kiungo wa kati wa Brighton aliyeshinda Kombe la Dunia la Argentina Alexis Mac Allister, 24, Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Mason Mount, 24, huku kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 21, akiwa ni mchezaji mwingine anayekaguliwa. (Liverpool Echo)

Mason Mount
Mason Mount
Image: GETTY IMAGES

Liverpool pia wanavutiwa na kiungo wa Feyenoord na Uturuki Orkun Kokcu, 22, kama mbadala wa Mac Allister na kiungo wa kati wa Dortmund Jude Bellingham, 19. (Footbal Transfers)

Manchester City wana nia ya kumsajili beki wa RB Leipzig na Croatia Josko Gvardiol huku klabu hiyo ya Ujerumani ikiomba £85m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mail)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 27, anasakwa na AC Milan ambao wanatazamia kujijenga upya kufuatia kushindwa kwao na Inter Milan katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Fabrizio Romano on Twitter)

Tottenham wameanza mazungumzo ya kumteua mkufunzi wa Feyenoord Mholanzi Arne Slot kama meneja wao mpya. (Football Insider).

Mshambuliaji Ivan Toney
Mshambuliaji Ivan Toney
Image: PA MEDIA

Kiungo wa kati wa Ecuador Kendry Paez ameripotiwa kusajiliwa na Chelsea kwa ada ya £20m huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 pia akivutia Manchester United. (El Canal del Futbol, via Mirror)

Brentford wanatazamiwa kuanza mazungumzo ya kandarasi na mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 27, mwishoni mwa msimu huu licha ya kufungiwa kwa miezi minane kutojihusisha na soka kwa makosa ya kamari. (Mail)

The Bees, wakati huo huo, wanataka kumsajili mshambuliaji wa Coventry City na Uswidi Viktor Gyokeres, 24, ili kufidia kutokuwepo kwa Toney kwenye timu. (Sport)

Kipigo cha jumla cha Real Madrid kutoka kwa Manchester City katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kinaweza kuongeza kasi ya kuondoka kwa bosi wao wa Italia Carlo Ancelotti. (Guardian)

Mkufunzi wa Real Mdrid Carolo Ancelotti
Mkufunzi wa Real Mdrid Carolo Ancelotti
Image: BBC

Bosi wa Swansea Russell Martin ni mmoja wa wagombea wanaoongoza kuwa meneja mpya wa Southampton. (Sky Sports)

Winga wa Brighton mwenye umri wa miaka 21, Simon Adingra anasakwa na vilabu vya Ujerumani na Ufaransa kufuatia kufanikiwa kwa mkopo Ubelgiji katika klabu ya Union Saint-Gilloise. ( 90min )

Sunderland wako kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili kiungo wa Birmingham Jobe Bellingham, 17, kakake mdogo wa mchezaji wa Borussia Dortmund na kiungo wa kati wa England Jude. (Sky Sports)

Mshambulizi wa zamani wa Wales Steve Morison, 39, anafikiriwa sana kurejea kama meneja wa Cardiff City - miezi minane baada ya kufutwa kazi na klabu hiyo. (Wales website)