SOKA KIMATAIFA

EPL: Nani wa kushuka daraja, nani atasalia

Baadhi ya timu tayari zimejisakia nafasi ya kushiriki ligi mabingwa.

Muhtasari

•Manchester City, Arsenal  na Newcastle United tayari zimekwisha kunasua nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa.

• Southampton tayari ikiwa imeyaaga mashindano hayo, Everton, Leicester na Leeds nazo pia hakuna iliyojihakikishiwa kusalia ligini.

tayari imeshushwa daraja kutoka EPL.
Southampton tayari imeshushwa daraja kutoka EPL.
Image: HISANI

Ligi kuu ya kandanda Uingereza itakuwa ikifika ukingoni wikendi ijayo huku timu tatu zikiwa katika hatari ya kushushwa daraja kutoshiriki msimu wa 2023/2024.

Baadhi ya timu  tayari zimejisakia nafasi ya  kushiriki ligi mabingwa pamoja na ile ya Ulaya huku zingine zikibakia wima katika ligi hiyo iliyojawa na ushindani mkubwa msimu huu.

Manchester City, Arsenal  na Newcastle United tayari zimekwisha kunasua nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa  huku Manchester United ikitazamaia  kuziba nafasi ya nne bora  iwapo  itapata sare dhidi ya Chelsea Alhamisi 25.

 Klabu ya Liverpool itakuwa ikipania kupata ushindi  katika mechi yake iliyobakia  na kuimboea Man U njaa katika mechi zake mbili  ndipo kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa.

Haya yanajiri huku timu ya Southampton tayari ikiwa imeyaaga mashindano hayo, Everton, Leicester na Leeds nazo pia hakuna iliyojihakikishiwa kusalia ligini kutokana na alama zao. Klabu za  Leicester na Leeds zina alama 31 ijapokuwa  Leeds United inadaiwa mabao mengi  kuishinda Leicester hivi kwamba, iwapo kwa mechi moja iliyosalia baina ya timu hizi mbili zitapata ushindi basi utofauti wa mabao utaamua gani ya kusalia.

Kwa upande wa timu ya Everton,  ambayo ina kibarua dhidi ya Bournemouth itakuwa ikihitaji ushindi au sare na kisha kuzitakia moja kati ya Leicester na Leeds kushindwa au kupata sare na hapo itakuwa ikipenya.

Hiki kitabakia kitendawili kinachodhamiriwa kuteguliwa baada ya kipenga cha mwisho wikendi, ndipo kubaini nani atakayekuwa akishiriki ligi hiyo msimu ujao, huku kufuzu kwa Newcastle na Arsenal katika nne bora kukiwaacha wengi vinywa wazi.