SOKA KIMATAIFA

Guardiola aeleza hofu yake katika matokeo dhidi ya Brighton

Walikunywa pombe yote katika Manchester

Muhtasari

•Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameeleza hofu aliyokuwa nayo katika matokeo ya mechi iliyochezwa Jumatano 24  dhidi ya Brighton mchwano wa ligi kuu Uingereza.

•Hili lilitokana na sherehe za unywaji pombe na ulevi walizoandaa vijana wake walipotwikwa taji la kwanza msimu huu siku chache zilizopita.

Pep Guardiola wa Manchester City
Pep Guardiola wa Manchester City
Image: GETTY IMAGES

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameeleza hofu aliyokuwa nayo katika matokeo ya mechi iliyochezwa Jumatano 24  dhidi ya Brighton mchwano wa ligi kuu Uingereza.

Hili lilitokana na sherehe za unywaji pombe na ulevi walizoandaa vijana wake walipotwikwa taji la kwanza msimu huu siku chache zilizopita.

Katika mitandao yake  ya kijamii Pep alisema, “ Nilikuwa na hofu kidogo jinsi tungepunguza alama baada ya saa 40 zilizopita ambapo tulikuywa pombe yote katika Manchester.”

Haya yanajiri baada ya matokeo ya 1-1  katika uga wa Falmer kilichochangia vijana hao wa Roberto De Zerbi kunasua nafasi kushiriki ligi ya Ulaya msimu ujao.“Brighton wamekuwa na mchezo mzuri msimu huu,waliichapa Arsenal 3-0 ugani Emirates, Manchester United na pia Chelsea ambazo ni baadhi ya timu kubwa.” Mhispaniola huyo aliendelea.

Baadhi ya wachezaji wa Man City hasa kiungo Grealish, Ruben Dias, Laporte, Akanji na wengine hawakuwa katika mchezo huo ijapokuwa watatarajiwa wikendi wakati ligi inafikia ukingoni dhidi ya Brentford kwa maandalizi ya fainali mbili zijazo.

City imekuwa mbioni kusaka mataji matatu msimu huu la muhimu likiwa la ligi ya mabingwa linalokusudiwa kuchezewa Juni 10 ambapo pia katika kombe la FA watakuwa na kibarua dhidi ya majirani wao Manchester United Juni 3.