Yanga ya Tanzania yaponyokwa na kombe la CAF licha ya kuilaza USM Alger 1-0

Licha ya kipigo hicho, Yanga ilipata faida kubwa ya fedha, kwani ilizawadiwa dola milioni moja.

Muhtasari

•Yanga ilihitaji kushinda mechi hiyo kwa tofauti ya mabao zaidi ya mawili ili kutwaa taji lao la kwanza kabisa kwenye Bara.

Image: BBC

Vigogo wa Tanzania, Yanga waliilaza timu ya USM Alger ya Algeria kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Julai 5 mjini Algiers Jumamosi usiku, lakini haikutosha kuwapa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, kwani walipoteza kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya jumla ya mabao 2-2.

Yanga ilihitaji kushinda mechi hiyo kwa tofauti ya mabao zaidi ya mawili ili kutwaa taji lao la kwanza kabisa kwenye Bara, lakini kipigo cha mabao 2-1 walichokipata nyumbani kilionekana kuwa na madhara huku Waalgeria hao wakitwaa taji hilo.

Alger ambao walikuwa wakicheza fainali yao ya pili ya Bara, walishinda taji lao la kwanza kabisa, na wakawa klabu ya kwanza kabisa ya Algeria kufanya hivyo.

Djuma Shabani ndiye aliyeifungia Yanga bao la kuongoza baada ya dakika saba tu kwa mkwaju wa penalti, lakini kampeni ya kupata bao la pili iliambulia patupu huku wenyeji wakiimarisha safu yao ya ulinzi.

Alger walikosa penalti kipindi cha pili wakati mlinda mlango wa Yanga raia wa Mali alipookoa juhudi za nahodha Zineddine Belaid, lakini haikuwasumbua kwani Yanga hawakuweza kupata bao la pili.

Licha ya kipigo hicho, Yanga ilipata faida kubwa ya fedha, kwani ilizawadiwa USD1mn (Sh137.7mn) kwa kutinga fainali huku washindi Alger wakiweka mfukoni USD2mn (Sh275.3mn).