Arsenal watoa ofa ya tatu ya £105m kumnunua kiungo wa West Ham

Siku ya Jumanne, West Ham pia ilikataa dau la pauni milioni 90 kutoka kwa washindi wa Treble Manchester City kwa ajili ya Rice,

Muhtasari
  • Mkataba wake wa sasa katika Uwanja wa London Stadium una chaguo la kuongezewa mwaka mmoja hadi msimu wa joto wa 2025.

Arsenal wamewasilisha ofa ya tatu yenye thamani ya £105m kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Uingereza Declan Rice.

Ofa mbili za kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 zimekataliwa baada ya fedha hizo kutofikia pauni milioni 100 walizotaka West Ham.

Hatahivyo, inaeleweka kuwa West Ham hawaamini muundo kwamba fedha walizopewa zinafaa

Siku ya Jumanne, West Ham pia ilikataa dau la pauni milioni 90 kutoka kwa washindi wa Treble Manchester City kwa ajili ya Rice, ambaye mkataba wake unaisha 2024.

Mkataba wake wa sasa katika Uwanja wa London Stadium una chaguo la kuongezewa mwaka mmoja hadi msimu wa joto wa 2025.

Kufuatia ushindi wa klabu hiyo kwenye Ligi ya Europa Conference dhidi ya Fiorentina mapema mwezi huu, mwenyekiti David Sullivan alisema ana uhakika wa "99%" Rice ataondoka West Ham msimu huu wa joto.