Mashabiki washangazwa na nzi anayemzunguka CR7 wakati wa mahojiano baada ya mechi

Licha ya kutumia kiganja chake kwa mara zaidi ya moja kumfukuza nzi huyo, alirudi mara kwa mara kwenye uso wake na hivyo kutatiza umakini wake katika mahojiano hayo.

Muhtasari

• Ronaldo alikuwa akifanya mahojiano hayo akiwa kazini Ureno wakati wa mechi za hivi majuzi za kufuzu kwa Uropa

Ronaldo,
Ronaldo,
Image: Instagram

Mashabiki wa mchezo wa kandanda wamepigwa na butwaa baada ya mchezaji Christiano Ronaldo kuonekana anasumbuliwa na nzi wakati wa mahojiano ya baada ya mechi yao kufuzu michuano ya Euro mwakani.

Nyota huyo wa Ureno ambaye ni maarufu sana na mara nyingi huwa na mashabiki wanaoomba picha au autographs zake hugonga vichwa vya habari hata kwa jambo dogo kama hilo la kuzungukwa na nzi.

Wafuasi wa CR7 wamefurahishwa baada ya video kuonekana ikionyesha nzi akimzunguka nyota huyo wa Ureno.

Nyota huyo wa Al-Nassr anaweza kuonekana akimzonga kila mara nzi huyo huku akijaribu kumfukuza wakati wa mahojiano.

Si mara moja, Ronaldo alionekana kutatizwa na nzi huyo aliyekuwa akirejea kwenye uso wake mara kwa mara licha ya kufanya juhudi za kutumia kiganja chake kumfukuza.

Mwishoni, Ronaldo mwenyewe aliona watu wamegundua kero la nzi huyo kwake na kutabasamu kwa kamera akiwa hana neno la kusema kuhusu nzi huyo asiye na stara kwa nyota mara 5 wa Ballon D’Or.

Ronaldo alikuwa akifanya mahojiano hayo akiwa kazini Ureno wakati wa mechi za hivi majuzi za kufuzu kwa Uropa.

Ureno ilifuzu kwa Ubingwa wa Uropa mwaka ujao ikiwa imesalia na michezo mitatu, shukrani kwa bao la kujifunga la Ronaldo dhidi ya Slovakia, BBC iliripoti.

Kufuatia video hiyo kufanya raundi, mashabiki wameitikia kwa furaha nzi huyo na njia zake za kuendelea.

Wengine walisema kwamba hii si mara ya kwanza kwa mdudu kuonekana anamzingira msanii huyo.

Inanikumbusha butterfly 🦋 katika fainali ya Euro." Mmoja alisema.

"Nzi Alitaka tu picha pia," mwingine alitania.