Wayne Rooney afunguka kuhusu uraibu wake wa pombe

Rooney aliibua suala la pombe kuwa moja ya changamoto ngumu zaidi

Muhtasari

•Rooney ameeleza katika kipindi kipya cha mtandaoni cha Rob Burrow kuhusu uhusiano wake na pombe katika siku za mwanzo za maisha yake ya soka.

Image: BBC

Nahodha wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney ameeleza katika kipindi kipya cha mtandaoni cha Rob Burrow kuhusu uhusiano wake na pombe katika siku za mwanzo za maisha yake ya soka.

Rooney alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na umri wa miaka 16 akiwa na Everton na haraka tu akawa maarufu.

Rooney, ambaye sasa ana umri wa miaka 38, alikuwa mgeni wa kwanza kwenye mfululizo wa kipindi kipya cha The Total Sport cha BBC kinachoendeshwa na Rob Burrow.

Alipoulizwa na Burrow kuhusu kukabiliana na changamoto katika maisha yake ya soka, Rooney, ambaye aliifungia England mara 53 na ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United, aliibua suala la pombe kuwa moja ya changamoto ngumu zaidi

Alimwambia Burrow: "Changamoto yangu ilikuwa pombe nilipokuwa na umri wa miaka 20. Nilikua nikinywa karibu kuzimia. Sikujua jinsi ya kukabiliana nayo. Sikutaka kuwa karibu na watu, kwa sababu wakati mwingine najihisi aibu."

Rooney, ambaye sasa ni meneja wa Birmingham City, anasema: "Usipotaka msaada na mwongozo wa wengine, unaweza kuwa katika hali ya mbaya sana, na nilipitia hali hiyo kwa miaka michache.

"Nashukuru, sasa siogopi kwenda kuzungumza na watu kuhusu jambo hili."