Wamiliki wa Man Utd wakosa kuhudhuria mazishi ya lejendari wa klabu, Sir Bobby Charlton

Familia ya Glazer, ambao kwa makusudi walikaa mbali na hafla hiyo kwa sababu hawakutaka kutoa usumbufu ambao haukukubaliwa kwa kupigiwa kelele na mashabiki.

Muhtasari

• Watu kadhaa mashuhuri walihudhuria mazishi yake wakiwemo Sir Alex Ferguson, Rais wa FA Prince William, bosi wa Uingereza Gareth Southgate, na Rais wa UEFA Aleksander Čeferin miongoni mwa wengine.

 
• Meneja wa zamani wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer pia alihudhuria, kulingana na The Mirror.

Image: BBC

Hafla ya kuuaga mwili wa gwiji wa Manchester United, Sir Bobby Charlton ilifanyika Jumatatu na wapenzi wa soka wenye vyeo na kutoka matabaka ainati walihudhuria.

Lakini katika msiba huo uliofurikwa na watu wakiwemo makocha wa zamani wa Manchester United, wachezaji wa zamani na viongozi wengine kwenye soka la Ulaya, ilibainika kwamba kocha wa sasa Erik Ten Hag na wamiliki wa klabu hiyo hawakuwepo katika msiba huo.

Sir Bobby aliaga dunia mwezi uliopita baada ya kuugua ugonjwa wa shida ya akili kwa muda mrefu, akiwa na marafiki, familia, na mashabiki waliokuwa wamepanga mitaa ya Manchester kutoa heshima kwa nyota huyo Jumatatu, Novemba 13.

Watu kadhaa mashuhuri walihudhuria mazishi yake wakiwemo Sir Alex Ferguson, Rais wa FA Prince William, bosi wa Uingereza Gareth Southgate, na Rais wa UEFA Aleksander Čeferin miongoni mwa wengine.

Meneja wa zamani wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer pia alihudhuria, kulingana na The Mirror.

Kama ilivyoripotiwa na GOAL, watu wengine mashuhuri waliokosekana kwenye mazishi hayo ni wamiliki wa Man United, familia ya Glazer, ambao kwa makusudi walikaa mbali na hafla hiyo kwa sababu hawakutaka kutoa usumbufu ambao haukukubaliwa.

Wachezaji wanne wa sasa wa Manchester United - Harry Maguire, Luke Shaw, Jonny Evans, na Tom Heaton - walikuwa kwenye orodha ya wageni na walifika kwenye mazishi.

Wachezaji wa zamani wa United, akiwemo Lou Macari, Bryan Robson, Mark Hughes, Brian McClair, Steve Bruce, Mike Phelan, Gary Pallister, Ryan Giggs, Peter Schmeichel, Andy Cole, Roy Keane, Nicky Buttt, Paul Scholes, Wes Brown, Wayne Rooney , Michael Carrick, Darren Fletcher, na Ashley Young pia walihudhuria.