Man City inapitia kipindi 'kigumu', asema Pep Guardiola baada ya kushindwa na Aston Villa

Washindi mara tatu hawajashinda katika mechi nne za ligi na wako pointi sita nyuma ya vinara Arsenal.

Muhtasari

•Baada ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Aston Villa Jumatano usiku meneja Pep Guardiola alikiri kuwa timu yake inapitia kipindi "kigumu".

•Takwimu hazionekani kuwa nzuri kwa timu ya Manchester City inayowinda taji lililovunja rekodi la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Premier.

Pep Guardiola wa Manchester City
Pep Guardiola wa Manchester City
Image: GETTY IMAGES

Nini kinaendelea kwa Manchester City?

Washindi mara tatu hawajashinda katika mechi nne za ligi na wako pointi sita nyuma ya vinara Arsenal kwenye Premier League.

Baada ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Aston Villa Jumatano usiku meneja Pep Guardiola alikiri kuwa timu yake inapitia kipindi "kigumu".

Naye mlinzi wa zamani wa Arsenal Martin Keown anaamini kuwa mabingwa hao wako "katika hali mbaya", akiambia BBC Mechi Bora ya Siku "wanaonekana hatarini".

Kombora la Leon Bailey dakika ya 74 lililopanguliwa liliipa Villa ushindi unaostahili - moja ambayo ilimaanisha City kuporomoka hadi nafasi ya nne kwenye jedwali, nyuma ya Villa, Liverpool na Arsenal.

Huku wapinzani wengi wakiibuka, je taji la City linaanza kutetereka baada ya mataji matatu mfululizo?

Takwimu

Ulinzi mbaya zaidi ulianza tangu 2009

Takwimu hazionekani kuwa nzuri kwa timu ya Manchester City inayowinda taji lililovunja rekodi la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Primia.

  • City wamecheza mechi nne za Primia League bila ushindi kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2017, wakiwa wametoka sare na Chelsea, Liverpool na Tottenham kabla ya kupoteza wakiwa na Aston Villa.
  • City iliruhusu mabao 17 katika mechi 15 za kwanza za Primia League kwa mara ya kwanza tangu 2009-10 walipomaliza nafasi ya tano.
  • Walijaribu mashuti mawili pekee dhidi ya Villa - mashuti machache zaidi kuwahi kufanywa na timu ya Guardiola katika mchezo ndani ya ligi kuu tano za Ulaya (michezo 535)
  • Mashuti 22 kutoka kwa Aston Villa ndiyo yaliyopigwa zaidi na Guardiola katika kipindi hicho.
  • Man City wamepoteza mechi zote nne ambazo Rodri hajacheza msimu huu
  • Inafaa kutaja ingawa katika msimu wao wa kushinda taji la 2018-19 chini ya Guardiola, City walikuwa pointi 10 kutoka kileleni baada ya michezo 19 na bado waliendelea kushinda Ligi ya Primia wakiwa na alama 98.