Afcon 2023: Tazama matokeo ya Jumamosi, ratiba ya michuano ya leo Jumapili

Ivory Coast walifungua kampeni yao ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau.

Muhtasari

•Seko Fofana aliiweka Ivory Coast kifua mbele katika dakika ya nne ya mchuano wa kwanza wa Kundi A ambao ulichezwa mjini Abidjan

walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Equatorial Guinea
Ivory COast walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Equatorial Guinea
Image: HISANI

Ivory Coast, ambao ni wenyeji wa  Kombe la Mataifa ya Afrika 2023  (AFCON 2023) walifungua kampeni yao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau.

Kiungo Seko Fofana aliiweka Ivory Coast kifua mbele katika dakika ya nne ya mchuano wa kwanza wa Kundi A ambao ulichezwa mjini Abidjan mwendo wa saa tano usiku, masaa ya Afrika Mashariki

Fofana alifanya majaribio mengine kadhaa ya kufunga kabla ya muda wa mapumziko lakini mlinda lango wa Guinea Bissau, Ouparine Djoco alikuwa rada.

Mshambulizi Jean-Philippe Krasso aliifungia Ivory Coast bao la pili baada ya kipindi cha mapumziko baada ya kudhibiti mpira kwa akili chini ya shinikizo kwenye eneo la goli. Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 58.

Fainali za Afcon za 2023 zimerudishwa nyuma kwa miezi 6 - mapema 2024, ili kuepuka msimu wa mvua katika eneo la Afrika Magharibi, lakini kuchelewa kulisaidia Ivory Coast kukamilisha maandalizi yao,na gharama ya jumla ya kuandaa zaidi ya Ksh bilioni 158.

Huku Ivory Coast wakitafuta ushindi wao wa tatu wa bara baada ya kushinda mwaka wa 1992 na 2015, ilibidi waanze harakati zao za kutafuta ubingwa bila mshambuliaji chaguo la kwanza Sebastien Haller kwa sababu ya jeraha.

Tazama Ratiba ya mechi za leo, Jumapili:-

Kundi A: Nigeria vs Equatorial Guinea, Alassane Ouattara Stadium, Abidjan (Saa kumi na moja jioni za Afrika Mashariki)

Kundi B: Egypt vs Mozambique, Felix Houphouet-Boigny Stadium, Abidjan (saa mbili usiku saa za Afrika Mashariki)

Kundi B: Ghana vs Cape Verde, Felix Houphouet-Boigny Stadium, Abidjan (Saa tano usiku saa za afrika Mashariki)