AFCON 2023: Raundi ya makundi yakamilika,tazama ratiba ya raundi ya 16 bora

Tunisia, Tanzania na Zambia waliungana na Algeria, Ghana, Gambia, Msumbiji na Guinea Bissau katika safari ya kurejea nyumbani.

Muhtasari

•AFCON 2023 imefika hatua ya 16 bora baada ya mechi za mwisho za makundi kuchezwa siku ya Jumatano usiku, Januari 24.

•Kufuatia mwisho wa hatua ya kikundi, ratiba ya kundi la 16 tayari imetoka.

Ratiba ya michuano ijayo
Image: CAF

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) inayoendelea nchinia Ivory Coast sasa imefika hatua ya 16 bora baada ya mechi za mwisho za makundi kuchezwa siku ya Jumatano usiku, Januari 24.

Mechi tatu kati ya zilizochezwa katika siku ya mwisho ya hatua ya makundi zilimalizika kwa sare ya 0-0 huku bao moja pekee likifungwa usiku wa Jumatano.

Namibia ilitoka sare ya 0-0 dhidi ya Mali, Afrika Kusini ikawa na matokeo sawa dhidi ya Tunisia, sawa na Tanzania dhidi ya D-R Congo. Morocco walipata bao pekee la usiku wa Jumatano lililofungwa na winga wa zamani wa Chelsea, Hakim Ziyech katika dakika ya 37.

Matokeo ya Jumatano yalimaanisha kuwa Tunisia, Tanzania na Zambia wangeungana na Algeria, Ghana, Gambia, Msumbiji na Guinea Bissau katika safari ya kurejea nyumbani. Guinea, Namibia, Mauritania na wenyeji Ivory Coast walipata bahati ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora baada ya kuibuka nambari tatu bora.

Kufuatia mwisho wa hatua ya kikundi, ratiba ya kundi la 16 tayari imetoka, iangalie hapa chini;

Januari 27  Angola vs Namibia

Januari 27 Nigeria dhidi ya Cameroon

 

Januari 28 Equatorial Guinea vs Guinea

Januari 28 Misri dhidi ya DR Congo

 

Januari 29 Cape Verde vs Mauritania

Januari 29 Senegal vs Cote d'Ivoire

 

Januari 30 Morocco dhidi ya Afrika Kusini

 Januari 30 Mali dhidi ya Burkina Faso