Eden Hazard amtupa Ronaldo chini ya basi na kumchagua Messi kama mkali wa Soka

Akiongezea, Hazard alisema kwamba ana uhakika wa asilimia mia kwa mia kwamba Neymar hawezi mfikia yeye katika ubunifu wa soka uwanjani.

Muhtasari

• Kwa miaka 15 iliyopita, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamepigana dhidi ya kila mmoja ili kuonekana kama mwanasoka bora zaidi katika historia.

Mess, Hazard and Ronaldo.
Mess, Hazard and Ronaldo.
Image: Facebook

Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Eden Hazard amemtupa chini ya basi lenye kasi Mreno Christiano Ronaldo huku akimchagua Muargentina Leonel Messi kama mchezaji mbunifu Zaidi duniani kuwahi kutokea, maarufu kama GOAT.

Akizungumza na gazeti la L’equipe, Hazard alisema kwamba licha ya wengi kuhisi Ronaldo ndiye mkali wao, kwake yeye ana mtazamo tofauti kwani anahisi Messi ndiye mchezaji mbunifu Zaidi ambaye ni vigumu kwa mchezaji yeyote kuweza kumpokonya mpira kutoka miguuni.

"Binafsi, Messi labda ndiye pekee. Nilipenda kumwangalia mchezaji wa Barcelona, ​​chini ya hapo mwishoni, lakini ndiye mkubwa zaidi katika historia. Haiwezekani kumpokonya mpira. Cristiano ni mchezaji mkubwa kuliko mimi lakini, katika historia. suala la soka safi, kiukweli sifikirii hivyo."

"Neymar, labda. Baada ya hapo, yeye si bora kuliko mimi, lakini kwa Real, umepata bora zaidi, pia kwa upande wa kazi zao: Benzema, Modric, walikuwa bora zaidi, Kroos, Kev' (De Bruyne), wote wanaonyesha soka,” aliongeza.

Kwa miaka 15 iliyopita, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamepigana dhidi ya kila mmoja ili kuonekana kama mwanasoka bora zaidi katika historia.

Mashabiki wa kandanda wa karne iliyopita watahisi kuwa ni Diego Maradona au Pele, wanaostahili lebo hiyo. Lakini mashabiki katika karne ya 21 wamekuwa wakibishana kuhusu Messi na Ronaldo.

Messi kwa sasa anafanya kazi na Inter Miami ya MLS, ambapo ameungana na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Luis Suarez, Sergio Busquets na Jordi Alba.

Wakati huo huo, Ronaldo yuko na klabu ya Saudi Pro League, Al Nassr. Kwa upande mwingine, Hazard alitangaza kustaafu akiwa na umri wa miaka 32 mwaka 2023, baada ya muda wa kukatisha tamaa akiwa na Real Madrid ya Uhispania, ambapo mara nyingi alishutumiwa kuwa mnene kupita kiasi na pia aliugua jeraha la kifundo cha mguu mara kwa mara.