Chelsea: Wamiliki kuwapa wachezaji marupurupu ya Ksh 92M wakishinda Carabao wikendi

Inaarifiwa wamiliki wapya wa Chelsea, Todd Boehly na Clearlake Capital wanachukulia Carabao kuwa taji la umuhimu mkubwa kwani endapo watashinda basi litakuwa taji la kwanza chini ya umiliki wao.

Muhtasari

• Kila mchezaji ambaye ameshiriki Kombe la Carabao msimu huu atapata mgao wa pesa, kulingana na dakika ngapi wamecheza.

• Ikiwa pesa zitagawanywa kwa usawa, kila mchezaji katika kikosi cha wachezaji 25 cha Pochettino atapata pauni 20,000.

Chelsea FC
Chelsea FC
Image: Facebook//CHELSEA FC

Wachezaji wa Chelsea wako katika foleni ya kupata bonasi iwapo watashinda fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Liverpool wikendi hii.

Ikiwa kikosi cha Mauricio Pochettino kitashinda ugani Wembley Jumapili, kikosi hicho kitagawana pauni 500,000 za bonsai [Ksh. 92,263,240.00].

Itakuwa ni ushindi wa kwanza wa kombe kuu tangu Todd Boehly na Clearlake Capital kuchukua mikoba kutoka kwa Roman Abramovich mnamo Mei 2022.

Wamiliki wapya wameweza kupunguza bili ya mishahara na wanafanya vibaya zaidi na malipo ya bonasi, ingawa wametumia zaidi ya pauni bilioni moja kununua wachezaji wapya katika miaka miwili iliyopita.

Chelsea wanaweza kuwa na wakati mgumu kwenye Premier League, lakini wamefanya vyema katika mashindano ya vikombe msimu huu.

The Blues ilizitoa Wimbledon, Brighton, Blackburn, Newcastle na Middlesbrough na kufika fainali ya Kombe la Carabao, huku wachezaji sasa wakiwa na nafasi ya kupata bonasi ya pesa.

Gazeti la Daily Mail limeripoti kuwa iwapo Chelsea itashinda, wachezaji hao watagawana kitita cha pauni milioni 500.

Kila mchezaji ambaye ameshiriki Kombe la Carabao msimu huu atapata mgao wa pesa, kulingana na dakika ngapi wamecheza.

Ikiwa pesa zitagawanywa kwa usawa, kila mchezaji katika kikosi cha wachezaji 25 cha Pochettino atapata pauni 20,000.

Manchester United, mabingwa wa Kombe la Carabao mwaka jana, waligawanya £1.6m kati ya timu. Mshindi wa msimu huu atapokea pauni 100,000 kutoka kwa EFL, huku Kombe la FA likitoa zawadi kubwa zaidi.

Chelsea hutoa bonasi nyingi kwa mafanikio ya Ligi ya Mabingwa, iwe ni kufuzu au kushinda shindano zima, kama walivyofanya Mei 2021.

Timu hiyo ya Stamford Bridge inatinga fainali ya Kombe la Carabao Jumapili baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Manchester City wikendi iliyopita.