Kocha afutwa kazi baada ya kumgonga 'headie' mchezaji wa timu pinzani Italia

D'Aversa alimgonga mshambuliaji wa Verona baada ya timu yake kupoteza kwa bao 1-0 kwenye Serie A.

Muhtasari

•Klabu ya Lecce ilitangaza kuachishwa kazi kwa D'Aversa siku ya Jumatatu ikisema, alikuwa ameachishwa kazi kufuatia tukio hilo.

imemfuta kocha Roberto D'Aversa.
Lecce imemfuta kocha Roberto D'Aversa.
Image: HISANI

Klabu ya Italia, Lecce imemfuta kazi meneja wake Roberto D'Aversa baada ya kumpiga kwa kichwa mshambuliaji wa Verona Thomas Henry kufuatia kichapo cha 1-0 cha Jumapili kwenye Serie A.

D'Aversa, 48, na Henry wote walipokea kadi nyekundu kwa upande wao kufuatia kisa hicho ambacho kilitokea huku hasira zikiwaka baada ya filimbi ya mwisho.

Akizungumza baada ya mchuano huo kwenye uwanja wa Stadio Via del Mare, bosi wa Lecce alikiri matendo yake "hayakuwa na kuruhusiwa"

 Klabu ya Lecce ilitangaza kuachishwa kazi kwa D'Aversa siku ya Jumatatu ikisema, alikuwa ameachishwa kazi kufuatia tukio hilo.

"Baada ya matukio yaliyotokea mwishoni mwa mechi ya Lecce-Verona, US Lecce inatangaza kwamba imemwachilia kocha D'Aversa kuacha majukumu yake. Shukrani zimwendee kocha na wafanyakazi wake kwa kazi iliyofanywa,” Lecce alisema katika taarifa yake.

D'Aversa alimgonga mshambuliaji huyo wa Verona baada ya timu yake kupoteza kwa bao 1-0 kwenye Serie A.

Bao la Michael Folorunsho la dakika ya 17 liliwafanya wageni kuwashinda Lecce na kuwasukuma hadi nafasi ya 15.

Lecce wameshinda mechi moja tu kati ya mechi 12 zilizopita za ligi ya Seria A, na kupoteza tisa katika kipindi hicho. Walimteua D'Aversa kuchukua nafasi ya Marco Baroni msimu uliopita wa joto.

D'Aversa alikuwa amesimamia Lecce tangu Juni, akishinda mechi sita pekee kati ya 30 kwenye usukani.