Maguire, Walker na Sam Johnstone waaga kambi ya Uingereza baada ya kupata majeraha

Watatu hao wameungana na washambuliaji Bukayo Saka na Harry Kane katika kuondoka kambi ya Uingereza.

Muhtasari

•Kipa Sam Johnstone na mabeki Harry Maguire na Kyle Walker wameondoka kutoka kambi ya Uingereza kutokana na majeraha.

•Kipa wa Burnley James Trafford na beki wa Man City Rico Lewis wameitwa kutoka kwenye kikosi cha vijana.

wameondoka kambi ya Uingereza kutokana na majeraha.
Harry Maguire, Sam Johnstone na Kyle Walker wameondoka kambi ya Uingereza kutokana na majeraha.
Image: X// ENGLAND

Kipa Sam Johnstone na mabeki Harry Maguire na Kyle Walker wameungana na mshambuliaji wa Arsenal Bukayo Saka na nahodha wa timu ya taifa Harry Kane kuondoka kutoka kambi ya Uingereza kutokana na majeraha.

Shirika la Soka la Uingereza mnamo siku ya Jumapili lilithibitisha kwamba wachezaji hao watatu waliondoka kambini na kurejea katika vilabu vyao kwa ajili ya kuchunguzwa baada ya kupata majeraha katika siku za hivi majuzi.

Timu ya taifa ya Uingereza imewatakia ahueni ya haraka.

"Kyle Walker, Sam Johnstone na Harry Maguire wamerejea katika vilabu vyao kwa kutathminiwa kuwa wamepata majeraha katika siku za hivi karibuni. Tunawatakia ahueni ya haraka vijana,” timu ya taifa ya Uingereza ilisema katika taarifa yake.

Kufuatia maendeleo ya hivi majuzi, Kipa wa Burnley James Trafford na beki wa Manchester City Rico Lewis wameitwa kutoka kwenye kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 kujiunga na kikosi cha wachezaji wakubwa.

Hapo awali, kocha wa Uingereza Gareth Southgate alikuwa amethibitisha kuondoka kwa mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane kutokana na jeraha aliloripoti nalo kwenye kambi ya timu ya taifa.

Bukayo Saka pia alikuwa amerejea katika klabu yake ya Arsenal mapema wiki iliyopita baada ya kuripoti kwenye kambi ya mazoezi akiwa na jeraha.

Timu ya Uingereza inasubiri kuwakaribisha Ubelgiji kwa mchuano wa kirafiki katika Uwanja wa Wembley siku ya Jumanne jioni, ikiwa ni mechi yao ya mwisho kabla ya mwisho wa mapumziko ya kimataifa.