Di Maria atumiwa ujumbe wa kumtishia maisha iwapo atarejeal klabu yake ya utotoni, Rosario

Tishio hilo lilikuwa ni jibu la taarifa ya awali ya Di Maria kwa TyC Sports: "Ningependa kurejea Rosario Central, mwaka huu au mwaka mmoja baadaye."

Muhtasari

•Ujumbe ulitumwa kwa familia yake ukiwatahadharisha kumuonya Di Maria dhidi ya uamuzi wa kutaka kurejea katika klabu yake ya utotoni.

Angel Di Maria
Angel Di Maria
Image: Instagram

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Manchester United na PSG, Angel Di Maria amepokea tishio la kifo ambalo halikutajwa jina, ambalo polisi katika mji aliozaliwa wa Rosario wanachunguza kwa sasa.

Angel Di Maria alipokea tishio la kifo ambalo halikujulikana aliyelituma kwake katika mji aliozaliwa wa Rosario siku ya Jumatatu.

Kwa sasa Di Maria yuko kwenye majukumu ya kimataifa na Argentina na wafanyikazi katika kondomu ya Funes Hills Miraflores, ambapo kwa kawaida hukaa anaporudi nyumbani, waligundua kifurushi kilicho na tishio hilo.

The Mirror wanaripoti kwamba Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, tishio hilo linamuonya Di Maria kutorejea katika klabu ya utotoni ya Rosario Central baada ya winga huyo mwenye umri wa miaka 36 kusema anatumai kumalizia soka lake huko.

"Mwambie mtoto wako Angel asirudi Rosario kwa sababu tutamuua mtu wa familia," tishio hilo lilisoma, kulingana na chombo cha habari cha Argentina Infobae.

"Hata [gavana wa mkoa, Maximiliano] Pullaro hatakuokoa. Hatuachi maelezo ya karatasi. Tunaacha risasi na watu waliokufa nyuma."

Tishio hilo lilikuwa ni jibu la taarifa ya awali ya Di Maria kwa TyC Sports: "Ningependa kurejea Rosario Central, mwaka huu au mwaka mmoja baadaye. Udanganyifu wa kurejea Gigante de Arroyito upo. Wakati huo utafika."

Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United kwa sasa yuko Benfica, lakini mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Licha ya tishio hilo, Di Maria anatarajiwa kuanza kuitumikia Argentina watakapomenyana na Costa Rica katika mechi ya kirafiki mjini Los Angeles.

"Di Maria anajua kwamba ana msaada wetu kamili kwa chochote anachohitaji," meneja Lionel Scaloni aliwaambia wanahabari. "Jambo muhimu ni kwamba anacheza, ambayo itampumzisha kidogo."