Rais wa zamani wa shirikisho la soka Uhispania akamatwa katika uchunguzi wa ufisadi

Aliwekwa kizuizini alipowasili Madrid kutoka Jamhuri ya Dominika.

Muhtasari

•Anashukiwa kupokea kamisheni kinyume cha sheria wakati wa kujadili dili nono la kuandaa mashindano ya Spanish Super Cup nchini Saudi Arabia.

•Baada ya kushuka kwenye ndege, aliingizwa kwenye gari jeusi na Walinzi waliokuwa wamevaa Kiraia.

Image: BBC

Luis Rubiales, rais wa zamani wa shirikisho la soka la Uhispania (RFEF), amekamatwa kama sehemu ya uchunguzi wa ufisadi.

Aliwekwa kizuizini alipowasili Madrid kutoka Jamhuri ya Dominika.

Anashukiwa kupokea kamisheni kinyume cha sheria wakati wa kujadili dili nono la kuandaa mashindano ya Spanish Super Cup nchini Saudi Arabia.

Bw Rubiales ambaye anakanusha makosa yoyote huenda akafungwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela.

Baada ya kushuka kwenye ndege, aliingizwa kwenye gari jeusi na Walinzi waliokuwa wamevaa Kiraia.

Polisi sasa wana saa 72 kumhoji Bw Rubiales, ambaye alikuwa katika Jamhuri ya Dominika wakati polisi walipopekua nyumba yake mwezi uliopita.

Pia walipekua makao makuu ya shirikisho la soka na kukamata watu kadhaa.

Bw Rubiales pia anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la unyanyasaji wa kijinsia kwa kumbusu mchezaji Jenni Hermoso mdomoni baada ya fainali ya Kombe la Dunia mwaka jana.

Bi Hermoso na wachezaji wenzake walisema busu hilo halikutakikana na lilidhalilisha.

Bw Rubiales alilazimika kujiuzulu, lakini amekanusha makosa yoyote